WATUMISHI MBEYA WAPEWA MATUMAINI KUHUSU KIKOKOTOO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 1, 2024

WATUMISHI MBEYA WAPEWA MATUMAINI KUHUSU KIKOKOTOO


NA MWANDISHI WETU, MBEYA

MKUU wa Wilaya aya Rungwe, Jaffar Haniu  amesema kutokana na mchango mkubwa wanaoutoa wafanyakazi mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla,  madai yao kwa  Serikali kuangalia upya suala la kikokotoo  litafikishwa mahali sahihi kwakuwa Serikali ya Awamu ya Sita ni sikivu na inawajali wafanyakazi.


 Haniu ameyasema hayo tarehe 1 Mei, 2024 akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani,  yaliyofanyika kimkoa wilayani Rungwe. 


" Tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani imekuwa ikiboresha mazingira ya kazi na kuwezesha wananchi wake kuingia  kwenye mfumo rasmi wa ajira serikalini, katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, hii inadhihirisha wazi kuwa inawajali wananchi wake", amefafanua Mhe. Haniu.


Ameeleza zaidi kuwa Serikali imeruhusu kuendelea kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, mkoa wa Mbeya  ukiwa umetengewa shilingi Bilioni 5.


Pamoja na hayo, Haniu amewataka wafanyakazi kupinga na kukemea vitendo vya rushwa katika maeneo ya kazi kwani palipo na rushwa  haiwezi kupatikana huduma bora.


Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi, Mratibu wa Chama cha Wafanyakazi TUCTA, Riziki Mashaka  alisema     mtumishi hufanya kazi kwa muda mrefu  bila ongezeko la mshahara wenye tija, kutokana na hali hiyo  hustaafu akiwa na kiasi kidogo cha fedha na kusababisha ugumu wa maisha kwa mtaafu huyo.


Amesema pia kuwa  kikokotoo kinamfanya mfanyakazi kupata fedha kidogo mara tu, anapostaafu kwa kupata asilimia 33 ya kile alichopaswa kukipata, hivyo ameiomba  Serikali kuboresha utoaji huduma kwa mifuko ya hifadhi ya jamii  ili wanufaika wapate stahiki zenye tija zitatakazo wasaidia kwenye kustaafu kwao, huku akitolea mfano kwa Wabunge wanaolipwa stahiki zao mara tu, wanapomaliza muda wao wawapo bungeni zaidi ya shilingi milioni 270 ikiwa ni nje ya mshahara wa kila mwezi.


Mashaka amesema kuna haja ya Serikali kubadili kanuni ili kunufaisha wafanyakazi na kuendelea kuimarisha zaidi mifuko ya jamii .




No comments:

Post a Comment