BODI YA SUKARI YATOA UFAFANUZI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, July 5, 2024

BODI YA SUKARI YATOA UFAFANUZI


NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Prof. Kenneth Bengesi, amesema wanaendeleza mchakato wa majadiliano na wadau wa sekta hiyo nchini lengo ni kuhakikisha maslahi ya umma na wadau yanalindwa.


Amefafanua hayo leo Julai 5, 2024 mbele ya Wahariri na Waandishi wa vyombo mbalimbali nchini na kuweka wazi anaamini kuwa majadiliano hayo yataweza kutatua changamoto zilizokitokeza na kusababjsha uhaba wa Sukari siku chache zilizopita na kufanya kuwepo kwa maneno mengi yanayoweza kuleta taharuki kama hakutakuwa na ufafanuzi kuhusu hali halisi ya kinachoendelea.

"Msimamo wetu na Serikali ni kuhakikisha wananchi, wakulima, wadau tofauti pamoja na wawekezaji wanalindwa na kuweka mazingira katika sekta hii yanayoendana na kukenga mahusiano mazuri kwa maslahi ya watanzania wote na kufanya maboresho kila inapohitajika kufanya hivyo," amesema.

Ameongeza kuwa sekta hiyo itafanya vema na kupata mafanikio zaidi kupitia majadiliano mbalimbali na wadau kwa maana jambo hilo ni nyeti na muhimu hivyo wanalichukulia kwa umakini kwa umakini mkubwa.


Siku chache zilizopita kumekuwa na mjadala mkubwa ndani ya Bunge na kusababisha kuleta hali ya sintofahamu nchini kuhusu mikataba kadhaa iliyodaiwa kusababisha uhaba wa  sukari nchini, ingawa ufafanuzi ambao umetolewa umeweka hali shwari.

Amefafanua kuwa wakati walipaoamua kulegeza mchakato wa uingizwaji wa sukari ilisababisha kuwepo kwa kiasi kikubwa kinachoingizwa nchini na kuyumbisha soko la ndani, hali iliyofanya Serikali kubadilisha Sheria na kubadili mfumo wa uingizaji wa bidhaa hiyo nchini jambo ambalo limesaidia kulinda soko la ndani.




 

No comments:

Post a Comment