NA HALIMA MWAMBA
KAMPUNI ya Heineken Beverage imeingia makubaliano na kampuni ya kitanzania Mabibo bia kwa ajili ya usambazaji wa bia ya Windhoek inayozatengenezwa nchini Namibia.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Mkazi wa Kampuni ya Heineken, Obabiyi Fagade amesema lengo la kuingia ushirikiano huo ni mkakati mahususi wa kusaidia biashara za ndani na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania na kupata fursa za ukuaji katika ya kusini mwa Afrika.
"Ushirikiano huo na Mabibo bia ,wines na spirits ni kufungua ukurasa mpya kwa kuunganisha utaaalamu wetu wa Kimataifa Kama Heineken na ujuzi mkubwa walionao katika soko la ndani,tuna uhakika katika uwezo wetu wa kuwasilisha bidhaaa na huduma za kipekeee kwa watej wetu Tanzania";,amesema .
Ameongeza kuwa Heineken imedhamiria kutoa huduma za kipekeee kupitia vinywaji vyenje ubora wa hali ya juu ambavyo vinakizi ladha ya watumiaji.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Bia, Jerome Rugelamalila amesema mkataba huo wa kibiashara umekuja baada ya kampuni ya Mabibo na Namibia Breweries kukubalina kuvunja mkataba walioingia mwak 2008 .
"Katika kipindi cha mwaka 1994 hadi 2012 tulikuwa tukifanya kazi na Heineken na sasa tumerejea tena kufanya kazi kwa pamoja hakika kwetu ni mafanikio makubwa na ninaamini tufafika mbali.
"Awali tulikuwa tunaingiza bidhaa kutoka nje na kusambaza na kutokana na kuadimika kwa dola hali ikawa nguvu, kwa sasa wao watakuwa wanaleta bidhaa hiyo hapa nchini na jukumu letu litakuwa ni kusambaza hivyo kwetu ni rahisi kwa mana tunauzoefu wa muda mrefu," amesema.
No comments:
Post a Comment