JOKETI AWAITA VIJANA KUZINDUA KAMPENI UWANJA WA BENJAMIN MKAPA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, July 4, 2024

JOKETI AWAITA VIJANA KUZINDUA KAMPENI UWANJA WA BENJAMIN MKAPA


NA MAGENDELA HAMISI

KATIBU Mkuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Taifa, Jokate Mwegelo ametoa wito kwa vijana wote Nchini  kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni inayohusu fursa zilizotengenezwa na zinazotengenezwa kwa vijana nchini.


Akitoa taarifa hiyo leo Julai 4, 2024 jijini Dar es salaam Joketi amesema uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika Julai 6, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.


" Kampeni hii kubwa ina lengo la kuhamasisha vijana kushiriki shughuli za kisiasa , kujiandikisha daftari la kudumu la wapiga kura litakalozinduliwa Julai 25 mwaka huu mkoani Kigoma" amesema 


Nakuongeza kuwa "Kampeni hiyo itazinduliwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Balozi Emmanel Nchimbi,hivyo vijana wote wajitokeze siku hiyo ili kufahamu fursa zilizotengenezwa chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.


Aidha ameongeza kuwa vijana ni wabunifu na wenye kuleta mawazo mapya ya kuinua na kuendeleza uchumi wa Taifa letu hivyo kupitia kampeni hii itasaidia kujadili fursa mbalimbali zinazowahusu vijana.

No comments:

Post a Comment