NA MAGENDELA HAMISI
JESHI la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limetangaza rasmi
kukamilika kwa maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuasisiwa kwake
Septemba Mosi 1964, chini ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere, yatakayoanza rasmi Julai
25,2024 na kuhitimishwa Agosti 23, mwaka huu.
Akitoa taarifa hiyo leo, Julai 3, 2024 mbele ya waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, Kaimu
Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda, maadhimisho
yashirikisha Kamandi zote za kijeshi ambazo zitafanya mazoezi katika nchi kavu
na baharini.
“Nawaomba wananchi kwa kipindi chote cha maadhimisho hayo makubwa wasiwe
na taharuki kwa kuwa ni ya kawaida ingawa yatakuwa ya kihistoria tangu
kuasisiwa kwa JWTZ na yatabaki vichwani mwa vizazi hadi kizazi,” amesema.
Luteni Kanali, Ilondo ambaye pia ni Msemaji wa Jeshi hilo amefafanua
kuwa za kijeshi zitakazokuwemo ni Jeshi la Anga, Jeshi la Wanamaji, Jeshi la
Nchi Kavu, Jeshi la Akiba, Jeshi la Akiba na Vikosi Maalumu
Pia ameweka wazi kuwa
majeshi hayo yatafanya mazoezi hayo ya maadhimisho katika katika mikoa ya Dar
es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Zanzibar sanjari hilo watakuwa
wakitoa huduma za kijamii kwa wananchi kupata vipimo na matibabu bure.
Katika nyanja ya matibabu,
tutaweza kupima magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza mfano, tutapima tezi
dume kwa njia ya damu, kisukari, presha, VVU, Shinikizo la juu na chini la
damu, pia tutahamasiha na kuchangia damu ili kuzipeleka kwa wahitaji maalumu
ikiwemo kwa akina mama wanaojifungua na kusaidia wananchi wanaopata ajali na
vituo vitakavyotumika ni vya Hospitali za Jeshi za Kanda ikiwamo Arusha, Mwanza,
Mbeya Tabora na Zanzibar na kwa Dar es Salaam Meli kubwa itatia nanga na kutoa
huduma za kimatiibabu kwa wananchi na itakuwa ni kama sehemu ya utalii na meli
hiyo itawasili Julai 16, mwaka huu na tunawomba wananchi wajitokeze kwa wingi”
amesema.
Ameongeza kuwa kutakuwa na vituo
vingine vya kutolea huduma ya matibabu katika maeneo mbalimbali nchini na kwa
Dar es Salaam, kituo kitakuwa Mbagala, Pwani kitakuwa eneo la Mapinga, Ruvuma
katika eneo la Luhiko, Pemba na Unguja.
Luteni Kanali Ilondo ameingeza
kuwa maadhimisho hayo pia yatahusisha gwaride kubwa litakolokuwa na sura ya
miaka 60 na kutakuwa na zoezi la pamoja kati ya Serikali ya Tanzania kupitia
JWTZ na Serikali ya Watu wa China kupitia, Jeshi la Ukombozi la Watu wa China.
Amefafanua kuwa zoezi hilo la
pamoja kwa majeshi hayo yatafanyika Julai 29, 2024 na kuhitimishwa 11, Agosti mwaka
huu na Tanzania ndio watakuwa wenyeji na litafanyika nchi kavu na baharini na lengo ni kuhadhimisha miaka 60 ya
ushirikiano wa pamoja kati waasisi wa mataifa ya Tanzania na China.
“Maadhimisho hayo yanafanyika chini ya Mkuu wa
Majeshi nchini na yatasimamiwa na Kamandi ya Nchi Kavu na wananchi wataweza
kuona zana mbalimbali za kivita zinazotumiwa na majeshi yetu katika kujilinda
na kuiweka nchi salama,” amesema.
Ameongeza kuwa katika maandimisho
hayo pia kutakuwa na Mashindano ya Mkuu wa Majeshi ya Utamaduni ambayo
yametokana na maono yake ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza nchini.
Tofauti na uwepo wa mashindano ya
utamaduni pia kutakuwepo kwa mashindano ya CDF ambayo yatatolewa maelezo zaidi
na kamati husika wakati wowote na wananchi watajulishwa.
No comments:
Post a Comment