MOBETO APATA UBALOZI BIDHAA YA SPAGETTH YA AZANIA GROUP - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, July 26, 2024

MOBETO APATA UBALOZI BIDHAA YA SPAGETTH YA AZANIA GROUP


NA MAGENDELA HAMISI

MWANAMITINDO Hamisa Mobeto, ametambulishwa kuwa Balozi wa bidhaa ya tambi aina ya Spaggethh inayotengenzwa na kampuni ya Azania Group.

Mobeto ametambulishwa leo, Julai 26, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Joel Laizer na kufafanua kuwa bidhaa hiyo ina miezi sita tangu kuingizwa sokoni. 

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Mobeto alisema kuwa alikuwa akiitumia bidhaa hiyo Kwa kipindi kirefu na ni furaha kwake kuwa Balozi na anaamini atafanya vema kuhamasisha jamii kuzitumia. 

"Naamini watanzania wataitumia kutokana a na ubora wa bidhaa tofauti na nyingine, hivyo nawaomba jamii kubwa wajitokeze kuitumia,"amesema. 

Awali Mkurugenzi, Laizer, alisema kuwa bidhaa hiyo inautofauti mkubwa na nyingine hivyo ni huu ndio wakati sahihi kuitumia.


"Hii bidhaa inaradha nzuri na haikamatiki kama nyingine hivyo ubora wake ni mkubwa tofauti na nyingine,"amesema


No comments:

Post a Comment