MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA ATIMIZA AHADI YAKE KWA CHUO CHA UFUNDI FURAHIKA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, August 6, 2024

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA ATIMIZA AHADI YAKE KWA CHUO CHA UFUNDI FURAHIKA


 NA HALIMA MWAMBA

MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM-Taifa), MNEC Rehema Sombi amekamilisha ahadi yake kutoa msaada wa Cherehani katika Chuo Cha Ufundi Stadi cha Furahika  ambacho kipo Buguruni Malapa lenmgo kuongeza ufasini wa ufundishaji kwa vitendo kwa wanafunzi wa fani ya ushonaji.

Msaada wa cherehani mbili zenye thamani ya Shilingi, 500,000 zimekabidhiwa leo Agosti 6, 2024 na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala, Juma Mizungu, kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo Taifa, Sombi ambaye hakuwepo katika makabidhiano hayo.

Sombi amekamilisha ahadi hiyo baada ya kuahidi kutimiz jambo hilo wakati wa mahafali ya 18 ya chuo hicho April, mwaka huu, pindi Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. David Msuya kueleza kuwa miongoni mwa changamoto chuoni hao ni upungufu wa vitendea kazi kwa ajili ya kufundishia wanafunzi ikiwemo cherehani.

Utekelezaji wa ahadi hii kutoka kwa Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa, Sombi, ni kutimiza lengo la kuwasaidia vijana hasa wanaosoma fani ya ushonaji ambapo kwenye mahafali yaliyofanyika hapa chuoni Aprili 27 mwaka huu, aliahidi kutoa cherehani mbili na tunashukru amekamilisha pia alifanikiwa kukabidhi fedha palepale sh. amesema Mizungu.

ameiongeza kuwa kubwa ambalo linatakiwa kufanyika kwa uongozi wa chuo hicho ni kuhakikisha cherehani hizo zinatuzwa vizuri kwa maslahi ya wanachuo na chuo kwa ujumla na akasisitiza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kuwa na uhusiano wa karibu na chuo hicho ili kufanikisha mpango wa utiaji elimu bure kwa vijana wa kitanzania.

Pia Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dkt David Msuya, amesema kwao ni furaha na faraja kuona ahadi ambayo iliyotolewa imetekelezwa kwa vitendo na jukumu limebaki kwao kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu stahiki ili waweze kujiari na kiajiriwa baada ya kuhitimu masomo yao.

Namshukuru sana mhe, Sombi kwa kutekeleza hili na tunaahidi kuzitunza ili ziendelee kutusaidia na kuwasaidia wanafunzi wengi zaidi na kuleta mafanikio yanayohitajika kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla pia niwaombe wadau wengine wana maendeleo kujitokeza kutusaidia vifaa vingine ikiwemo kompyuta, amasema.

Pia amesema kwa sasa wameanzisha programu kwa ajili ya akina mama kusoma masomo ya ushonaji kwa muda wa jioni, hivyo amewaomba kundi hilo kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha kuwainua kiuchumi baada ya kupata ujuzi huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mivinjeni,Kata ya Buguruni Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo ndipo kilipo Chuo  Cha Furahika, Fadiga Legele amesema wao kama viongozi wanafarijika kwa uwepo wa chuo hicho na wataendelea kutoa ushirikiano Kama serikali ya Mtaa na Kuwa mabalozi wa Chuo hicho.


"Katika mikutano yetu na wananchi, tunajipanga kuwaita viongozi wa chuo hiki ili waeleze fursa zinapatikana kwa vijana ili iwe chachu kwa kundi hili kujiunga na masomo Jambo litakalowaondoa katika tabia hatarishi," amesema.






No comments:

Post a Comment