NA MWANDISHI WETU, SONGWE
MAHAKAMA ya Wilaya ya Momba Imemhukumu Esau Andrew Hinjo, aliyekuwa Askari wa SUMA JKT-TUNDUMA adhabu ya kwenda Jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh. 500,000/- kwa kosa la kuomba na kupokea Hongo Kinyume na Kifungu cha 15(1) (a) na 2 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 Marejeo ya Mwaka 2022.
Hukumu dhidi ya Esau Andrew Hinjo imetolewa katika Kesi ya Rushwa Na.23763/2024 Agosti 21, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mh. Claud Msenjelwa wa Mahakama ya Wilaya ya Momba.
Kesi hiyo imeendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU , Lilian Matara.
Ilielezwa kuwa Mshtakiwa alifikishwa Mahakamani kwa shtaka la Kupokea Hongo Kiasi cha sh.120,000/- toka kwa Joseph Itera Chunche kama kishawishi cha yeye kutokamata nyavu haramu za kuvulia Samaki.
Mshtakiwa alikiri makosa yake na kulipa faini ya sh.500,000/-
%20(1).jpeg)




No comments:
Post a Comment