NFRA KUNUNUA TANI MILIONI 1.7 ZA NAFAKA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, August 10, 2024

NFRA KUNUNUA TANI MILIONI 1.7 ZA NAFAKA


NA MWANDISHI WETU, DODOMA

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umesema kuwa umepanga kununua tani milioni 1.75 za nafaka mbalimbali kutoka kwa wakulima hapa nchini kwa ajili ya mauzo ya ndani na nje ya nchi.


Kati ya tani hizo, NFRA tayari imeshasaini mkataba wa kuuza tani 1,150,000 katika nchi za Jamhuri ya Congo (DRC) na Zambia na zilizobaki ni kwa ajili ya soko la ndani.


Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma jana, Mkurugenzi Mkuu wa NFRA, Dkt Andrew Komba amesema kuwa tani 650,000 za mahindi zimeshaanza kusafirishwa kwenda nchini Zambia toka wiki iliyopita baada ya malipo kufanyika.


Amesema kuwa tani nyingine 500,000 zimenunuliwa na Serikali ya Congo (DRC) kwa ajili ya jimbo la Katanga nchini humo.


Amesema, ukichialia mbali kuuza nafaka hizo nchini DRC na Zambia,  NFRA pia ipo katika utekelezaji wa mkataba wa kuiuzia nafaka shirika la Chakula  Dunia (WFP) ambazo wanazipeleka nchini Malawi.


Amesema WFP waliomba kuuziwa tani 100,000 lakini wameanza na mkataba wa kuchukua tani 35,000 kwa sasa.


“Hii inaonyesha hitaji kubwa la nafaka kwa mwaka huu kwa ajili ya mauzo ya ndani na nje ya nchi na tumejipanga vizuri kukidhi mahitaji ya soko hilo,” amesema Dkt Komba.


Katika hatua nyingine,Dkt Komba amesema kuwa NFRA ina mpango wa kununua tani zipatazo laki 6 za Mahindi na Mpunga kutoka kwa wakulima katika utaratibu wake wa kawaida wa kuhifadhi chakula na baadaye kukiingiza katika mzunguko.


Kati ya tani hizo, tani 500,000 ni za Mahindi na tani 100,000 ni za Mpunga.


Amesema ununuzi wa nafaka hizo ni kwa ajili ya usalama wa chakula ambapo tani 500,000 ni za Mahindi na zilizobaki ni za Mpunga.


“Lengo ni kuiwezesha nchi kuwa na hifadhi ya kutosha ya chakula,”


“Lakini pia kuziuza nafaka hizo kwa wananchi wenye mahitaji pale watakapohitaji,” amesema.


 NFRA  ipo imara na itekeleza matarajio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inayolenga kumkomboa mkulima kwa kununua mazao yao kwa  bei nzuri na furahia matunda ya kazi yao na kuongeza kipato.


No comments:

Post a Comment