NA HALIMA MWAMBA
TAASISI ya Sambaza Upendo, Amani na Umoja Tanzania kesho itafanya shughuli maalumu ya kuliombea taifa, Rais Dkt Samia na viongozi wote na familia zao kwa lengo la kuendelea kulifanya taifa kuwa na amani aliosisiwa tangu uhuru.
Mwenyekiti wa Sambaza Upendo, Amani na Umoja ambaye ni Mbeba Maono, Askofu Dkt Leonard Ntibanyiha amesema ufunguzi wa shughuli hiyo itaanza mchana na dua itakayoongozwa na Sheikh Salehe Rashid huku maombi yataongozwa na Askofu Mwasota.
Pia amefafanua kuwa awali mgeni rasmi walipanga awe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na kutokana na majukumu aliyonayo kimkoa atawakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko.
“Kesho ndio siku ya kusambaza upendo katika maeneo ya Kigogo na tunaamini wapo watu wanaostahili kupewa sadaka, na shughuli hii itafanyika Kigogo Post katika Msikiti wa Jumuia ya Shia Ith na Sheria (TIC), hivyo tunawaomba wananchi kutokeza kwa wingi ili kuomba kwa pamoja taifa kwa ajili ya maslahi ya Watanzania wote ,” amesema.
Pia amesema watatoa sadaka ya nguo kwa makundi maalumu hususan kwa wahitaji kupitia makundi maalumu yakiwemo ya wazee waishio katika mazingira magumu, Watoto Yatima na Wajene ambao wapo katika eneo hilo la Kigogo Kituo Cha Polisi, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment