NA HALIMA MWAMBA
TAASISI ya Sambaza Upendo, Amani na Umoja Tanzania wamewafaraji wajane, watoto Yatima wazee na wanaoishi katika mazingira magumu wa eneo la Kigogo Post jijini Dar es Salaam.
Hayo yamefanyika leo, Ijumaa Agosti 2, 2024 kwa kutoa misaada ya vitu mbalimbali ikiwemo nguo za thamani kama suti, pamoja na vinywaji na kufurahia nao lengo likiwani kudumisha amani na upendo kwa jamii hiyo yenye mahitaji.
Sheikh Mohamed Abdi ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Jumuia ya Shia Tanzania (TIC), akimwakilisha Kiongozi Mkuu wa Msikiti huo na Jumuia ya Shia Ith ambako shughuli hiyo imefanyika, Hemed Jalala, amesema jambo linalofanywa na Sambaza Upendo ndio maelekezo ya Mungu.
“ Huu ni ujasiri mkubwa ambao mmefanya kuja kufanya shughuli hii hapa katika msikiti huu, wengine wanashindwa hata waislamu wenzetu wanashindwa lakini nyinyi mmeweza kwa kweli Mungu atawalipa mema zaidi.
“Pia haya ambayo mmefanywa leo ndio Mtume wetu Mohammad (S.A.W) alisistizwa kuyafanya mbele ya jamii pale alipoambiwa na Mungu“ Nakuhamlisha ukawe na huruma kwa viumbe vyote wakiwemo wanyama, ndege, binadamu na ukafungamane vizuri na watu, “alinukuu.
.Ameongeza kuwa “Ukimuona kiongozi wa dini anahubiri mapambano hayo ni yake, sio dini inavyotaka, hivyo sisi tunapinga machafuko yoyote yanayoendelea duniani, mfano ukanda wa Gaza tunaamini wanaongamia wapo ndugu zetu katika imani na wengine ambao tunahitaji kuwa wamoja ili kuiweka dunia salama.
Amekumbuka kuwa duniani kuna watu wawili tu, mmoja ni nduguyo kiimani na wa pili ni mtu mwenye umbile kama wewe kwa maana ni binadamu mwenzako, hivyo kama hupendi kudhurumiwa naye hapendi kudhurumiwa, kama hupendi kuteseka naye hapendi kuteseka hivyo ni jambo la msingi kuoneana huruma kama ambavyo wanafanya Sambaza Upendo.
Ameongeza kuwa si kinyaa Muislamu kukaa na Mkristo kujumuika pamoja katika shughuli mbalimbali ikiwemo sherehe na msiba na shughuli nyinginezo lengo likiwa ni kudumisha na kusambaza upendo ili kuendeleza amani na utulivu kitaifa na kimaifa.
Naye Msoma Risala, Mchungaji Marry Mudirikati kwa niaba ya Mwenyekiti wa Sambaza Upendo, Amani na Umoja ambaye ni Mbeba Maono wa taasisi hiyo, Askofu Dkt Leonard Ntibanyiha amesema kuhamasisha upendo unafanyika kwa kukumbushana na kuelimishana kwa maana msingi wa Tanzania umejengwa na upendo.
Amesema mwaka 1958 kabla ya uhuru wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Nyerere alisema kuwa “ Hatuweza kutengeneza roketi tukaipeleka mwezini kama mataifa makubwa yanavyofanya bali tunatatengeneza roketi ya upendo na matumaini hapa nchini na kuisambaza duniani”, alinukuu.
Ameongeza kuwa kutokana na msingi huo hakuna budi kwa watanzania bila kujali tofati za dini zao wanawabijika kuwa na upendo na amani kwa wakati wote na kuwa mfano kwa mataifa mengine kukimbiliana kwa shida na raha na ndio sababu ambayo imewasukuma kutoa misaada hiyo kwa wahitaji.
No comments:
Post a Comment