WAKANDARASI WA MRADI WA TAZA kV 400 WATAKIWA KUKAMILISHA KAZI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, August 17, 2024

WAKANDARASI WA MRADI WA TAZA kV 400 WATAKIWA KUKAMILISHA KAZI


NA MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Nishati,  Dkt. James Mataragio ameongoza kikao cha Tatu cha Kamati ya Uongozi ya Mradi wa TAZA kV 400 kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. 


Kikao hicho kilichofanyika Leo, Agosti 17,kilijadili utekelezaji wa mradi wa TAZA hadi kufikia Julai, 2025 kimewataka wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo kukamilisha kazi mapema kwa mujibu wa mkataba. 


Mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa TAZA unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia (TAZA), vituo vya kupoza umeme vya Iringa, Mbeya, Tunduma na Sumbawanga pamona na mfumo wa kutoa huduma ambao utawezesha kuunganisha Bara la Afrika kwa nishati ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia. 


Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na taasisi zake pamona na Wizara ya Fedha.





No comments:

Post a Comment