DC MPOGOLO AWAITA WANANCHI KONGAMANO LA ELIMU YA KUGAWA MIKOPO YA SH. BIL 14 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, November 9, 2024

DC MPOGOLO AWAITA WANANCHI KONGAMANO LA ELIMU YA KUGAWA MIKOPO YA SH. BIL 14


NA MWANDISHI WETU 

MKUU ww Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kongamano la wazi kuhusu elimu ya mikopo ya asilimia 10 inayotarajiwa kuanza kutolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.


Mpogolo amesema kiasi cha sh. bilioni 14 zimetengwa kwaajili ya mikopo hiyo kwa vikundi  vya wajasiriamali wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Amesema kongamano hilo linaambata na maonesho ya bidhaa za wajasiriamali, litafanyika Novemba 11 -12 mwaka huu.


“Tutatoa elimu muhimu ya kuhusu mikopo hii tunayotarajia kutoa. Pia elimu ya nishati safi. Hivyo ninawaomba wananchi wake kwa wingi Mnazi Mmoja siku hiyo,” amesema Mpogolo.


Ameeleza,  kongamano hilo ni muhimu kwani litatoa elimu ya kutosha kuhusu mikopo hiyo, elimu ya matumizi, urejeshaji  na elimu ya nishati safi.


“Nikongamano kubwa  na litapambwa na maonyesho na burudani mbalimbali. Wananchi waje kushiriki,” amesema Mpogolo.

No comments:

Post a Comment