Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbuya, akizungumza katika mahafali hayo.
NA MAGENDELA HAMISI
UONGOZI wa Chuo cha Kodi (ITA) umetakiwa kuendelea na kutoa mafunzo kwa
Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yanayohusu makusanyo ya kodi
katika sekta maalumu za kiuchumi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbuya akimwakilisha
Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba, ametoa wito huo leo, Novemba 22, 2024
jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 17 ya ITA ambapo wahitimu 417
aliwatunuku vyeti katika ngazi tofauti za elimu.
“Ni jukumu la chuo kuendelea kutoa mafunzo haya kwa watumishi wa TRA
ili kuwajengea uwezo na weledi kwa lengo
la kuwawezesha kubaini vyanzo vipya vya kodi na kuhakikisha kila kodi
inayostahili kulipwa, inalipwa kwa wakati sahihi.
“Katika hili mnabidi mzidishe mafunzo hususan kwenye utozaji kodi katika biashara mtandao na za kimataifa ambazo kwa sasa zinaendelea kushika kwa kufanya hivyo mtakuwa mmeisaidia Serikali kuokoa mapato ambayo yalikuwa yanapotea kutoka katika sekta hiyo kutokana na kukuwa na wataalamu wa kutosha katika eneo hilo,” amesema.
Ameongeza kuwa eneo hilo linatakiwa kupewa kipaumbele kwa kuwa ufanyaji biashara kila wakati ubadirika ulimwenguni hivyo Serikali inahitaji kuona biashara zinazofanyika mtandaoni zinafanyika ipasavyo na kodi stahiki inakusanywa ipasavyo.
Mwandumbuya kwa niaba ya Waziri Nchemba akasisitia kwamba ITA ni vema ikaangalia uwezekano wa kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara ya namna ya wanavyoweza kujisajiri na kulipa kodi eneo hilo ambalo linaonekana kuwa na changamoto katika ulipaji wa kodi.
Ameongeza kuwa ni matarajio ya Wizara kuona jitihada za ITA katika kutoa mafunzo ya forodha na kodi yanachangia Serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa maana inahitaji rasilimali fedha kutoka vyanzo tofauti vya mapato kwa kuzalisha vijana wenye weledi wa kukusanya mapato na kutoa ushauri wa kodi.
Pia ametoa wito kwa ITA kufanya tafiti zitakazojielekeza kutatua changamoto hususan katika mifumo ya forodha na kodi nchini kwa lengo la kujenga mfumo bora wa kodi ambao urahisisha ulipaji kodi kwa hiari.
“Naamini tafiti hizo zitasaidia kuibua vyanzo vipya vya mapato, udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato jambo litakaloongeza wigo wa makusanya ya mapato nchini na tifiti zikitufikia tutazifanyia kazi ipasavyo,” amesema.
Ameongeza kuwa kwa uzoefu ambao wanao jamii inahitaji uwepo wa mazingira rafiki ya ulipaji kodi na wanaelewa wajibu wao katika hilo, pia wanapenda kushirikishwa katika utunzi wa sheria au mabadiliko yanayotokea.
Pia wengi wanapenda kuona kodi zinazishushwa ingawa hawatoi njia ya nini Serikali ifanye kufidia upungufu baada ya viwango vya kodi kushushwa na tafiti nyingine zinakosa takwimu zinazoweza kuwashawishi watunga sera na sheria kuendana zinazotolewa.
“Hivyo chuo mje na tafiti zitakazosaidia kuleta mapendekezo yatakayoibua na kutupeleka katika kufikia malengo ya kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia makusanyo ya kodi,” amesema.
Mkuu wa Chuo cha Kodi, Prof. Isaya Jairo, amesema chuo hicho kimefanikiwa kuzalisha wataalamu wenye umahiri katika masuala ya forodha na kodi, wakilenga kukuza uchumi wa Taifa kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa.
“Tumetoa mafunzo ya mkakati kwa wafanyakazi 7,438 hadi sasa, kuhakikisha
wanakuwa na ujuzi wa kukabiliana na changamoto za ukusanyaji wa kodi,” alisema
Prof. Jairo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda, naye
ameleza kuwa mamlaka hiyo itaendelea kuboresha miundombinu ya chuo hicho ili
kuhakikisha kinazalisha wahitimu bora kwa maendeleo ya nchi.
“Pia tunaangalia uwezekano wa kupanua mafunzo ya lazima kwa wafanyakazi
wa ngazi za juu kama sehemu ya mkakati wa kuongeza idadi ya walipa kodi na
kuimarisha ulipaji wa kodi,” aliongeza Mwenda.
Mwenda, katika mahafali hayo amewataka wahitimu hao
kuendeleza umahiri kutokana na mafunzo ambayo wamepata chuoni hapo na
wajitokeze kwa wenye kwenye kuomba nafasi za kazi TRA.
Ameongeza kuwa hivi karibu TRA inatarajia kutangaza
nafasi za kazi, hivyo kwenye usahili wanatakiwa kuonesha uwezo ili waoate
nafasi za kazi na wala hatapendelewa mtu, uwezo wake ndio utasababisha kupata
kazi.








No comments:
Post a Comment