TWAHA TWAIBU, AUSTRIA
BALOZI na Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria, Naimi Azizi amefungua maonesho ya utalii ya kutangaza utalii wa Tanzania yanayojulikana kama ' My Tanzania Road Show' yanayofanyika mjini Vienna, Austria
Aidha,Maonesho haya yanafanyika katika upande wa mashariki na magharibi mwa Bara la Ulaya katika nchi za Ujerumani, Jamhuri ya nchi ya Czchec, Austria na Poland.
Maonesho yalianza Novemba 11,2024 katika mji wa Frankfurt,Ujerumani na baadaye yakafanyika katika mji wa Prague , Jamhuri ya Czchec na Novemba 13, yamefanyika mji wa Vienna, Austria na yamehitimishwa jana Novemba 15, 2024 katika mji wa Warsa nchini Poland
Washiriki wa maonesho hayo kutoka Tanzania ni baadhi ya Taasisi za Serikali zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii (TAWA, TANAPA Na NGORONGORO) na Kampuni za watu binafsi za utalii(Tour operators).Maonesho haya yameratibiwa na Kampuni ya Utalii ya Kili Fair iliyopo jijini Arusha.
Katika hotuba ya Balozi Azizi aliyetoa jijini Vienna,Austria kwa washiriki wa maonesho hayo wakiwepo kampuni zaidi ya 57 yanayojihusisha na Utalii nchini Austria, ameyakaribisha kampuni hizo kuleta watalii na kuwekeza nchini Tanzania.
Pia ameelezea uhusiano na ushirikiano mzuri wa diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na nchi hiyo.









No comments:
Post a Comment