MISAADA YA WAATHIRIKA KUPOROMOKA GHOROFA KARIAKOO ITOLEWE KUPITIA AKAUNTI YA MAAAFA - DKT YONAZI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, November 18, 2024

MISAADA YA WAATHIRIKA KUPOROMOKA GHOROFA KARIAKOO ITOLEWE KUPITIA AKAUNTI YA MAAAFA - DKT YONAZI


NA MWANDISHI WETU


KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia walioathirika wa kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam itolewa kwa akaunti maalumu ya maafa ya 9921159801 ambayo ipo Benki Kuu ya Tanzania na kushughulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.



Dkt. Yonazi ameyasema hayo leo Novemba 18, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali inayoendelea katika zoezi la uokoaji.



Amesema akaunti hiyo ni pekee nchini ambayo inakusanya misaada ya kifedha kwa ajili ya maafa.



"Kuna watu wana nia njema kabisa ya kuwasaidia Watanzania, lakini naomba tujizuie kabisa kukusanya michango ya kifedha kutoka kwa mtu yeyote bila kupitia akaunti hii". Amesema Dkt. Yonazi.


Aidha amesema akaunti hiyo ni maalumu imethibitishwa na Serikali ili kuweza kuhakikisha misaada inawafikia walengwa na inatimiza malengo ya kutoa misaada hiyo.


Amesema kwa sasa operesheni inaendelea mpaka pale watakapokamilisha zoezi la kuokoa baadhi ya watu ambao bado hawajaokolewa.









No comments:

Post a Comment