NA MWANDISHI WETU
OFISI ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa imepokea, Shilingi milioni 20 kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa lengo la kusaidia shughuli za uokoaji katika Jengo la ghorofa ambalo limeporomoka Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Jenerali Mstaafu George Waitara ambaye pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, amekabidhi hundi hiyo leo, Novemba 21, 2024 kwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu DKT. Jimmy Yonazi.
Kabla ya kukabidhi hundi hiyo, Jenerali Waitara amesema kwamba Watanzania wasiwe na taharuki Nna wanachotakiwa ni kupata taarifa sahihi kutoka mamlaka husika na kwingine ili Kupata taarifa sahihi.
" TANAPA ni sehemu ya wananchi wa Tanzania,hivyo janga hili tumetugusa tukaona tutoe chochote kusaidia uokoaji wa maafa haya na Watanzania wasiwe na taharuki kwani tumeona shughuli za uokoaji zinakwenda vizuri, kikubwa wawe wanafuatilia taarifa kupitia mamlaka husika na si vyanzo vingine " amesema Jeneral Waitara.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu DKT. Jimmy Yonazi ameishukuru TANAPA kwa msaada huo,nakuwaomba Watanzania walioguswa na maafa hayo waendelee kutoa michango yao ili kufanikisha zoezi la uokoaji kwa haraka.
Pia ametangaza 'Control Number 'kwa ajili ya kuwawezesha wananchi ambao wataguswa Asda haya kutuma michango yao kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji.
" Control number ni 987320001709 ambapo namba hii inatumika kwa mitandao yote ,mwananchi anaweza kuchangia kuanzia 1000 nakuendelea na fedha hizi zinaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya Maafa ambayo ni 9921159801" amesema Dkt.Yonazi.









No comments:
Post a Comment