JOHN TENDWA AFARIKI DUNIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, December 16, 2024

JOHN TENDWA AFARIKI DUNIA




MSAJILI wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, anasikitika kutangaza kifo cha John Bill Tendwa, aliyewahi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuanzia mwaka 2001 hadi 2013. 

Tendwa amefariki dunia leo, Desemba 17, 2024, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. 


Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa na familia kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Kibamba Hospitali. 


Ratiba na taarifa rasmi za mazishi zitatolewa mara baada ya kukamilika. 


Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi.

No comments:

Post a Comment