VETA WAINGIZA SOKONI BUNIFU 13 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, December 2, 2024

VETA WAINGIZA SOKONI BUNIFU 13

Meneja Uhusiano kwa Umma Veta, Sitta Peter, (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari, kulia ni kufundushia mfumo wa jua na muundo wa Atomu, Ernest Malanya.

MAGENDELA HAMISI


CHUO cha Ufundi Stadi VETA Dar es Salaam Katika kipindi cha miaka  mitano kimefanikiwa kuibua bunifu 118 na kati ya hizo 13 zimeingizwa sokoni na 45 zipo katika mchakato wa kuingizwa sokoni.


Meneja Uhusiano kwa Umma Veta, Sitta Peter, amebainisha leo, Desemba 2, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tisa la ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu pamoja na Maonesho yanayofanyika jijini humo kwa siku tatu.


Ameongeza kuwa Katika bunifu hizo zipo dawa za fangasi, UTI na ya kuzuia mbu waenezao malaria na kufafanua kuwa vema Watanzania wakazitumia ili kuwaongezea hamasa za kuendelea kubuni dawa nyingine.


"Leo tupo katika maonesho haya ili kuwaonesha watanzania na jamii Kwa ujumla na ambavyo tumeweza kufanikiwa katika kufundisha na kubuni bidhaa ambazo zinaweza kuwa msaada kwa jamii kulingana na changamoto zinazowakabili," amesema.


Naye, Alli Issa ambaye ni Mwalimu wa Chuo cha Veta Dar es Salaam, amesema kutokana na kufanikiwa kubuni bidhaa mbalimbali wa tayari wamezipatia hati miliki ili bunifu hizo zisiweze kuchukuliwa au kuigwa na wengine.


"Pia kwa bidhaa ambazo bado hatujaziingiza sokoni tunaendelea na mchakato wa kupata miliki bunifu, naamini tutafanikiwa" amesema.


Naye Mvumbuzi wa kifaa cha kufundushia mfumo wa jua na muundo wa Atomu, Ernest Malanya, amesema tayari kifaa hicho kimepata ruhusa ya kufundishia kwenye shule za msingi na sekondari baada ya kupata Ithibatia kutoka Wizara ya Elimu.


Kutokana na hilo, Malanya ambaye pia amewahi kuwa mwanafunzi hicho, ametoa ombi kwa Serikali na wadau wa elimu kumsaidia mtaji ili aweze kutengeneza kifaa hicho kwa wingi jambo litakalosaidia kufikia malengo ya kutawanywa kwenye shule mbalimbali nchini.


"Nimefanya kazi kubwa Katika kubuni kifaa hiki na ninaamini wanafunzi wengi wataweza kuelewa vizuri somo la mifumo ya jua, hivyo naomba wa elimu wanisaidie mtaji ili niweze kutengeneza kifaa hiki kwa wingi," amesema.




No comments:

Post a Comment