NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa wito kwa wakazi wa Temeke na vitongoji vyake kuanza kufikiria kumiliki Bima ya Afya na kuacha kuweka fedha kwa ajili ngoma (vigodoro).
Chalamila amebainisha hayo leo, wakati akizundua huduma ya upimaji afya kwa wakazi wa Temeke na vitongoji inatolewa kwa siku tano kuanzia leo Januari 13 hadi 17, 2025.
Huduma hiyo inatolewa kupitia Kambi ya Matibabu inayotokewa na madaktari Bingwa wabobezi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, amefafanua kwamba huduma za kimatibabu zitakazotokea katika viwanja ya hospitali hiyo ni uchunguzi wa magonjwa ya moto, mfumo wa mkojo, saratani ya mlango wa kizazi na mengineyo.
Nduguzanguni lazima niwaeleze ukweli wapo baadhi ya watu wanawekeza fedha zao kwaajili ya kucheza ngoma 'vigodoro' , wengine kwaajili ya kufanya starehe mbalimbali wakisahau kuwekeza kwenye afya.
"Kibaya zaidi unaweza kutumia fedha nyingi leo na kesho yake ukaanza kuumwa na kuhitaji fedha kwa ajili ya kupata matibabu, hapo unaweza kujiuliza kipi bora kuwekeza ili utubiwe wakati huna pesa au utumie fedha kwenye starehe,"alihoji.
Ameongeza kuwa " nawaombeni ndungu zangu mfahamu kuwa afya ni muhimu kuliko starehe ambazo mnazifanya Kwa kuwekeza fedha nyingi na kusahau kukata bima ambayo itatumika kukutibia wakati huna kitu na utaachana na kuomba misaada ili utubiwe.
Hapa leo kuna mabingwa wa magonjwa mbalimbali mtawaona wote Kwa yule anayehitaji, kikubwa mnapaswa ni kuchangia kidogo na hicho unachangia kinakwenda kuleta huduma nyingine kama vile maji, umeme, dawa na nyinginezo.
Pia ameongeza kuwa kutokana na madaktari hao mabingwa kufika kutoa huduma ni jambo la kumshukuru Rais Samia kwa kujali afya za watanzania.
Amefafanua kuwa huduma ambazo wanatoa mabingwa hao, sehemu nyingine zinapatikana kwa gharama kubwa tofauti na kuchangia kwa gharama ndogo kwa kipindi hiki cha kambi, hivyo ni vizuri wakajitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo.
.png)




No comments:
Post a Comment