MEGAWATI 30 JOTOARDHI KUINGIA KWENYE GRIDI IFIKAPO 2026/27 - DKT KAZUNGU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, January 13, 2025

MEGAWATI 30 JOTOARDHI KUINGIA KWENYE GRIDI IFIKAPO 2026/27 - DKT KAZUNGU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt Khatibu Kazungu akizungumza kwenye mkutano mkuu wa muunganiko wa nchi kwenye masuala ya jotoardhi una iendelee mjini Abu Dhabi

NA MWANDISHI WETU, UAE

IMEELEZWA kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye rasilimali kubwa ya uwekezaji miradi ya jotoardhi  ambapo jumla ya megawati 30 zinatarajiwa kuingizwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo mwaka 2026/2027


Hii inafuatia uwepo wa  Megawati 5000 za umeme na Megawati 15000 za Joto Kwa ajili ya matumizi ya Moja Kwa moja  kwenye miradi ya jotoardhi.


Hayo yameelezwa  Januari 14, 2025 na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia umeme na nishati jadidiifu Dkt Khatibu Kazungu wakati wa mkutano mkuu wa muunganiko wa nchi kwenye masuala ya jotoardhi yaani Global Alliance ambao umefanyika kwenye baraza kuu la 15 la IRENA.


Kazungu amesema kuwa  Tanzania inatarajia kuwa miongoni mwa nchi ambazo zinaongoza kwenye uendelezaji wa  umeme wa jotoardhi Kusini mwa Jangwa la Sahara.


Akinadi fursa ziilizoko nchini Tanzania katika mjadala wa ngazi ya juu  kwenye mkutano huo, Dkt Kazungu amesema rasilimali hiyo ya jotoardhi inachagizwa na uwepo wa mikondo miwili ya Bonde la Ufa la Afrika Mashariki ambacho ndicho chanzo kikuu Cha Nishati hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki.


‘’ Tanzania imeainisha maeneo 50 ambayo  yana viashiria vya uwepo wa rasilimali ya jotoardhi  katika mikoa takribani 16 ya nchi yetu,  maeneo hayo yapo katika hatua mbali mbali za uendelezaji kwa ajili ya uzalishaji umeme na fursa ya matumizi ya moja Kwa moja.’’ Amesema Dkt Kazungu


Aidha  ameongeza kuwa Tanzania inawakaribisha wabia wa maendeleo, taasisi binafsi  kuwekeza Tanzania ili kuweza kuchangia upatikanaji wa nishati safi ya uhakika, endelevu na rafiki wa mazingira


Aidha amesisitiza kuwa pamoja na uwepo wa vyanzo hivyo, pia serikali kupitia kampuni ya Uendelezaji Joto Ardhi Tanzania TGDC ambayo ni kampuni tanzu ya TANESCO, imetoa kipaumbele Kwa miradi mitano ya kimkakati ili kuweza kuharakisha upatikanaji wa nishati hiyo, miradi hiyo ni pamoja na ule wa Ngozi-MW 70, Kiejo mbaka 60MW iliyopo mkoani Mbeya, Songwe-MW 38 iliyopo mkoani Songwe na Luhoi-MW 5 iliyopo mkoani Pwani,  ambapo Miradi hii ipo katika hatua ya uhakiki wa rasilimali ,na Mradi wa Natron wa Megawati 60 mkoani Manyara ambao upo katika hatua ya utafiti wa kina. 


Ameongeza kuwa pindi niradi hiyo itakapoanza kuzalisha umeme itachagiza uchumi wa nchi, kutunza mazingira na kuongeza kipato cha mwananchi mmoja mmoja kupitia upatikanaji wa ajira.


 Amesema kwa sasa Tanzania inajipanga kuhakikisha  miundombinu, ushirikishwaji wa sekta binafsi  na wabia wa maendeleo wanapewa kipaumbele kwenye utekelezaji wa miradi hii ambayo ni rafiki kwa mazingira.





No comments:

Post a Comment