MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF)
Taifa, Prof Ibrahim Lipumba ameteua, Rajab Mbarouk Mohamed kuwa Katibu wa
Kamati ya Itifaki na Udhibiti ya chama hicho.
Pia amemteua, Juma Wandwi kuwa
Naibu Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibit na wataanza kazi mara moja na
watathibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kikao kijacho na uteuzi wa wakurugenzi
wengine utatangazwa kwa kadri uteuzi utavyokamilika.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa
leo Jan. 13, 2024 na Kitengo cha Habari ya chama hicho na ikafafanua kwamba, Prof.
Lipumba amefanya uteuzi huo kwa kuzingatia Katiba ya CUF- Chama Cha Wananchi ya
mwaka 1992 Toleo la 2019, Ibara za 91(1) na 92(1).
No comments:
Post a Comment