MWENYE MASHAKA NA MAAMUZI YA MKUTANO MKUU AJE KWANGU- WASIRA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, January 26, 2025

MWENYE MASHAKA NA MAAMUZI YA MKUTANO MKUU AJE KWANGU- WASIRA


NA MWANDISHI WETU

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mainduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema uamuzi wa Mkutano Mkuu ambao umemchagua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kutetea kito chake katika Uchaguzi Mkuu ujao ni zingatio la Katiba na si vinginevyo.

 

Amebainisha kwa kuna maneno kutoka kwa baadhi ya wanaojiita wanaCCM wakidai kuwa bado hawajaelewa sababu ya wajumbe wa mkutano huo kupitisha uamuzi huo, hivyo atawasaidia kuelewa kwani uwezo wa binadamu kufahamu jambo hauwezi kulingana.

 

Hayo ameyasema leo Januari 26, 2025 jijini Dar es Salaam alipozungumza na viongozi, wanachama, wapenzi wa CCM na wananchi kutoka maeneo mbalimbali walipojitokeza kumpokea.

 

"Baada ya Mkutano Mkuu kutambua kazi kubwa ambazo zimefanywa Serikali zote mbili, ya Muungano na ya Mapinduzi Zanzibar, Mkutano Mkuu wa CCM ukasema kama hali ni hii kuna sababu gani kuchelewesha kutangaza mgombea?.

 

"Sasa wapo watu wanaosema wao ni wanachama wa CCM, hawakuelewa. Hilo nalo siyo jambo la ajabu. Tutawasaidia kuelewa maana siyo watu wote wanaweza kuelewa sawa. lakini tunawaambia Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya CCM ndiyo kikao kikuu cha mwisho," amesema.

 

Pia amesema kwamba Mkutano Mkuu wa Chama una mamlaka ya kubadili, kufuta na kurekebisha uamuzi wowote uliofanywa na kikao cha chini yake, kufuta maamuzi yaliyofanywa na kiongozi yeyote wa CCM.

 

"Sasa aliye na mashaka katika jambo hilo kama wote hawawezi aje kwangu nitamsadia maana katiba ipo kichwani. Uamuzi tulioufanya umezingatia Katiba ya CCM ibara ya 101 inayotutaka tuchague jina moja la kuwa mgombea wa kiti cha Urais, tulitumia ibara hiyo na kwa mamlaka ya Mkutano Mkuu ameteuliwa Dk. Samia.

No comments:

Post a Comment