NA MWANDISHI WETU
SERIKALI imesema
ipo tayari kuunga mkono juhudi ambazo zimeoneshwa na mwigizaji katika tasnia ya
filamu nchini, Irene Uwoya, kuptia kampeni yake ya kuhamasisha wanawake
wanaofanya shuguli za kilimo wasikate tamaa.
Hayo
yamebainishwa leo jijini Dar esn Salaam na Angela Kairuki ambaye ni Mshauri wa
Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan wakati uzinduzi wa kampeni ya Kuhamaisha wanawake
ambao wanaofanya kilimo wapige hatua na wasikate tamaa ambao inaongozwa na
Uwoya.
“Pongezi kwa
Uwoya na kama Serikali tuko tayari kumuunga mkono katika kampeni yake ya
kuhamasisha wanawake ambao wamo katika sekta ya kilimo waendelee kufanya hivyo
ili kuhamasisha wengine kuingia humo kwa maana inaendeleza juhudi za rais wetu
kuendeleza sekta ya kilimo,” amesema .
Rais wetu Dkt Samia,
ameifungua nchi kupitia sekta ya kilimo kwa kufanya kazi kubwa kwa kuiboresha na
kusababisha wakulima kufanya vizuri ingawa miaka ya nyuma ilionekana wanaoingia
katika nyanja hiyo kama wanadharauliwa.
Pia amesema Dkt
Samia, ameweka fedha kwa ajili ya mikopo kwa wakulima kupitia Serikali imeweka
fedha za kutosha ilihali miaka ya nyuma wakulima walikuwa wanashindwa kuaminika
kukopeshwa kupitia benki ila kwa sasa hali ni shwari.
Tofauti ha hilo
wakulima wemekuwa wakipatiwa elimu inayosaidia kupata ,mbinu mbalimbali za kuboresha
ili kuendana na mabadiliko yanayohitajika kupitia sekta ya kilimo kwa lengo la
kufikia mafanikio yenye tija.
Kairuki ameongeza
kwamba Serikali imefanikisha kupatikana kwa masoko ndani na nje ya nchini kusaidia
wakulima kutosumbuka kutafuta pa kuuzia mazao yao na kinachotakiwa kwa sasa ni
wakulima kufuata kanuni za kuhakikisha mazao bora yanapatikana ili kuwa na soko
la uhakika.
Pia ameongeza
Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Rais Samia, imefanikisha kujenga mahusiano
bora ya kimataifa jambo linalosababisha wakulima kupata mafunzo kadha wakadha
yanayofanya kuwa na kilimo bora kwa maslahi ya wakulima na nchi kwa ujmla.
Naye Uwoya alitanabainisha kwamba siri kubwa
ya mafanikio yake ameyapata kupitia kilimo jambo linalofanya watu wengi
kumuuliza maswali mengi kuhusu mafanikio na baadhi yao wakihoji yametokana na
nini.
“Takribani miaka
sita sasa, jamii kwa ujumla ilikuwa ikijiuliza mafanikio yangu yametokana na
nini, hivyo leo nimeona niwajibu kwa kwamba kilimo ndio kimefanya nipate mafanikio,
hivyo ombi kwa wanawake wengine waje wajiunge kwenye kilimo, ingawa kinachangamoto,
kikubwa ni kuvumilia”, amseema.
Uwoya
ambaye ni Mwenyekiti wa mradi huo ameendelea kusema kuwa ameamua kuanzisha
Mradi huo kutokana na yeye binafsi kuwekeza kwenye sekta ya Kilimo ambapo amefanikiwa
kufanya kilimo Cha Tangawizi pamoja na Mpunga huko Mbarali Mkoani Mbeya.
Amesema
kuwa kwa Sasa sekta ya Kilimo imepiga hatua kubwa kutokana na Serikali kuwekeza
kwenye sekta hiyo kwa kuwezesha wakulima kupata pembejeo za kilimo,Zana Bora za
Kilimo pamoja na Mikopo ya kuwawezesha katika kilimo.
"
Toka nianze kujihusisha na kilimo Mwaka 2018 ,nimeona Mapinduzi makubwa sana
ndani ya sekta ya kilimo,namshukuru sana mama yetu na Rais Wetu Dkt
Samia,pamoja na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa jitihada hizi wanazizifanya
katika kuleta Mapinduzi ya Kilimo" amesema
Nakuongeza
kuwa Sekta ya Kilimo ni muhimili muhimu katika pato la Taifa,nakwamba Serikali
imekuwa ikiweka mazingira rafiki katika kukuza sekta hiyo kwa kuweka jitihada
muhimu ikiwemo kusimamia kilimo cha kisasa, kutoa pembejeo za kutosha,kutafuta
masoko ya uhakika kwa ajili ya wakulima kuuza mazao yao,pamoja na kutoa Mikopo
kwa wakulima wadogo.
Amesema
kwamba asilimia 67 ya wanawake ndani ya familia wanajihusisha na
kilimo,asilimia 29 ni wanaume ndani ya familia wanajihusisha na kilimo,pia
asilimia 4 pekee ni wanawake na wanaume ndani ya familia wasiojihusisha na
uzalishaji wa aina yoyote.
"Jembe
ni Mama" ni kampeni ambayo nimeanzisha kwa ajili ya kusaidia Wizara ya
Kilimo kuwa na kilimo bora chenye maslahi kwa wanawake wakulima nchini
Tanzania" amesema Uwoya.
No comments:
Post a Comment