NA MWANDISHI WETU, PWANI
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) Mkoa wa Pwani, katika kipindi cha mwaka 2024/24 imefanikiwa kukagua
miradi ya Maendeleo 167 yenye thamani ya zaidi ya shilingi, bilioni 43,342,632,386.86
na lengo likiwa ni kuhakikisha fedha za Serikali zinatumika kikamilifu.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Christopher
Mzava ameweka wazi hayo leo, Januari 20, 2025 na kufafanua kuwa ukaguzi huo
ulifanyika katika Ofisi zake tisa za Mkoa huo ambazo ni Mafya,Kisarawe,
Bagamoyo, Rufiji Mkuranga, Kibaha Vijijini, Kibaha Mji, Ikwiriri, Chalinze na
Kibiti.
Amesema miradi 32 imekaguliwa katika ofisi
iliyopo Mafya,ya thamani ya sh. bil. 5.3, Ikwiriri miradi 10 ya zaidi ya sh.
Bil 1 na laki 6, Chalinze miradi nane ya sh. bil 3 na laki 2, Kibiti miradi 25
ya sh. bil 3.8 na Pwani katika Halmashauri mbili ya Kibaha Mji na Vijijini
miradi 26 yenye thamani ya sh.bil 6.1 na Bagamoyo tulikagua miradi 18 yenye
thamani ya sh. bil 3.9, Kisarawe miradi 13 ya sh. bil 5.3, Mkuranga miradi 25
ya bil 12.2, Rufiji miradi 10 ya sh. bil 3.5, " amesema.
Pia amesema pamoja hayo kuna miradi mingine
bado inaendelea kukamilishwa ukiwemo wa Bagamoyo miradi 18, Kisarawe miradi
minne, Mkuranga 23, Rufiji mitano, Mafya miradi14, Ikwiriri miradi nane,
Chalinze miradi minne, Kibiti miradi yote 24, Pwani miradi yote 26.
"Tunafanyaje kwamba Serikali inatoa fedha
nyingi kwa ajili ya kuwaletea Maendeleo wananchi, tukiwa kama Takukuru lengo
letu ni kuhakikisha kwamba zile fedha zinatumika kikamilifu amesema.
Ameongeza kuwa katika kuongeza ufanisi wa
shughuli zao wanashirikiana na wananchi vizuri kupitia programu ya Takukuru
Rafiki, jambo linalosaidia kupata taarifa za changamoto zinazojitokeza kwenye
jamii na kuzifanyia kazi.
Pia ameweka wazi kuwa milango ipo wazi kwa
wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa taasisi hiyo kuhusu masuala ya rushwa
katika miradi mbalimbali inayoendelea ili hatua ziendelee kuchukuliwa kwa
wahusika ili kuokoa fedha za Serikali zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya
maendeleo.
No comments:
Post a Comment