TAWA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA UTALII NA USAFIRISHAJI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, January 16, 2025

TAWA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA UTALII NA USAFIRISHAJI


NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inashiriki mkutano wa kimataifa wa Utalii na Usafirishaji unaofanyika Dubai, Falme za Kiarabu ambao umeanza tarehe 15/01/2025 na unatarajia kumalizika leo tarehe 16/01/2025.


 Mkutano huo ambao umeandaliwa na Taasisi ya Teknolojia na Utafiti ya barani Asia (ITAR) unahudhuriwa na washiriki kutoka takribani nchi 52 duniani kote


Katika Mkutano huo ambao unalenga kuonyesha mapinduzi ya kiteknolojia katika tasnia ya utalii na usafirishaji na kubadilishana mawazo baina ya washiriki wa mkutano huo kwa ajili ya kuboresha sekta ya utalii na usafirishaji, TAWA inawakilishwa na Mhifadhi Mwandamizi Kelvin Fella ambaye ni Kamanda wa Hifadhi ya Magofu ya Kilwa. 


Kupitia Mkutano huo SC. Kelvin Fella amefanya wasilisho kuhusu namna miundombinu ya kitalii na usafirishaji iliyofanywa na TAWA inavyosaidia ukuaji wa utalii katika Hifadhi ya Kilwa. Aidha Sc. Fella aliezea kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Kilwa Kisiwani na Songomnara ambayo ni Urithi wa Dunia  na kuwasilisha shughuli za utalii zinazofanyika Kilwa pamoja na kuwakaribisha wageni kutoka mataifa mbalimbali kutembelea Kilwa na Tanzania kwa ujumla. 


Mbali na kuelezea utalii wa Kilwa Sc. Fella alitangaza shughuli za utalii katika maeneo mengine yanayosimamiwa na TAWA pamoja na fursa za uwekezaji katika shughuli za utalii wa uwindaji na kugawa vipeperushi kwa washiriki wa mkutano huo. Aidha aliwasihi washiriki hao kuchangamkia fursa hizo na kuwa mabalozi wazuri wa TAWA.




No comments:

Post a Comment