CHALAMILA KUSHUHUDIA 'KNOCKOUT YA MAMA' - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, February 27, 2025

CHALAMILA KUSHUHUDIA 'KNOCKOUT YA MAMA'


NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert  Chalamila anatarajia kuwaongoza Watanzania kushuhudia mapambano ya ngumi yasiyokuwa ya kuwania mkanda yanayopigwa leo, Feb 28 katika Ukumbi wa Magomeni Sokoni jijini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimepatikana wakati mchakato wa kutambulisha mabondia watakaotwangana leo katika ukumbi huo, kwamba Mkuu wa Mkoa huo, Chalamila atakuwa miongoni mwa viongozi watakaokuwemo ukumbini humo kushuhudia mapambano hayo.

"Wakati tukiendelea 'Face Off' kwa mabondia watakaopigana (kesho), leo nimepata taarifa kuwa Mkuu Wetu wa Mkoa anatufuatilia kupitia mitandao ya Kijamii ambayo ipo mubashara kwa sasa na ameahidi kuwepo kushuhudia," alisikika mmoja wa washehereshaji alisema.


Mchakato wa kutambulisha mabondia hao lililokwenda sanjari na tambo kutoka kwa mabondia ilisababisha bondia Abdallah Pazzy 'Dullah Mbabe' almanusura azichape kavukavu na mpinzani wake.


Pambano la linatazamiwa kwa hamu kubwa na kuvuta husia za mashabiki wengi ni kati ya mtoto wa Rashid Matumla Snake Man', Amiri Matumla dhidi ya Mnamibia, Pauls Amavila ambalo litakuwa 'Main Card'

Mkurugenzi wa Mafia Promotion, Ally Zayumba, akizungumza baada ya tukio hilo, amesema kutakuwa na mapambano 14 Kwa mabondia wa ndani na nje ya nchi kuoneshana ubabe.

Ameongeza kuwa huo ni msimu wa tatu wanaandaa mapambano hayo 'Knockout ya Mama' lengo kubwa ni kuunga mkono juhudi anazofanya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza michezo na kunadi miradi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita. 

"Tuna kila sababu ya kumshukuru Rais Dkt Samia kwa kutubeba katika michezo, wengi mmeshudia kuna goli la Mama, pia amefanya mengi katika sekta ya masumbwi nasi tunandaa mapambano haya ili kuunga mkono juhudi zake," amesema.


Awali kabla ya mchakato wa 'showface' kufanyika jioni ya jana Feb 27, 2025 mabondia hao walipata nafasi ya kupima uzito asubuhi na viingilio ni 50,000, 20,000 na 10,000


No comments:

Post a Comment