NA MWANDISHI WETU
MAFIA Boxing Promotion imeendelea na juhudi za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, kuondokana matumizi ya Nishati ya Mkaa baada ya kugawa majiko ya gesi kwa Mama Ntilie wa Magomeni Sokoni, jijini Dar es Salaam.
Mama Ntilie hao zaidi ya 30, wamepatiwa majiko hayo leo, Feb 27, 2025 wakati wa kuwatambulisha mabondia 14 watakaopanda ulingoni kesho Feb, 28 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Magomeni Sokoni.
Akizungumza baada kugawa majiko hayo Kwa Mama Ntilie hao, Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion, Ally Zayumba, amesema wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha wanaunga mkono harakati za Rais Samia za kuondokana na matumizi ya nishati chafu kwa watanzania.
"Rais wetu, Dkt Samia amekuwa akihamasisha watanzania kuachana na matumizi ya nishati chafu ambayo ni mkaa na kuni, nasi tukaona hatuna budi kuunga mkono jitihada hizo kwa kugawa majiko kwa Mama Ntilie wenye mahitaji katika soko hili la Magomeni, amesema.
Baadhi ya Mama Ntilie ambao wamepata majiko hayo ni Zubeda Idd, Anna Joseph, Halima Tumbo, Shufaa Abras, Rehema Singa, Zarau Omari, Asha Bindu, Theresia Vincent na wengineo.
Pia Asha Bindu kwa niaba ya wenzake ameishukuru Mafia Boxing Promotion kwa kuwapa majiko hayo, kwani itawasaidia kupika kwa haraka na Kwa muda mafupi
"Tunawashukuru Mafia Boxing Promotion kwa kutupa majiko hayo kwani yatatusaidia kufanya vema katika mapishi yetu na kuendana na muda," amesema.





No comments:
Post a Comment