HALMASHAURI YA MJI KIBAHA YAHITIMISHA MAFUNZO WAANDIKISHAJI WASAIDIZI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, February 11, 2025

HALMASHAURI YA MJI KIBAHA YAHITIMISHA MAFUNZO WAANDIKISHAJI WASAIDIZI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


NA MWANDISHI WETU, KIBAHA PWANI

WAANDIKISHAJI wasaidizi wa zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura Halmashauri ya Mji Kibaha wametakiwa kuwa waadilifu na waaminifu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.


Hayo yamesemwa na Ofisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Dk Rogers Shemwelekwa alipokuwa akifunga mafunzo ya siku mbili kwa waandikishaji wasaidizi kwenye Halmashauri hiyo.



Shemwelekwa amesema kuwa waandikishaji hao wasaidizi wamepewa jukumu kubwa na wameaminiwa kwani zoezi hilo ni la Kitaifa hivyo wahakikishe wanalifanya kwa weledi ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza.


Amesema mafunzo hayo yawe chachu ya utendaji kazi wao kwenye zoezi la uboreshaji taarifa za wapiga kura na kuandikisha wapiga kura wapya litakuwa la siku saba kuanzia Februari 13 hadi 19.


Amewataka watumie lugha nzuri wakati wakiwahudumia wananchi ili iwe sehemu ya kuwavutia watu wengi wajitokeze kuboresha taarifa zao na kuandikisha wapiga kura wapya.


Jumla ya waandikishaji 262 wamepatiwa mafunzo hayo na kuna vituo 131 vitatumika kwenye zoezi hilo ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu.

No comments:

Post a Comment