NA MWANDISHI WETU
KAMATI Kuu ya Chama cha National League for Democracy (NLD), inakutana kesho, Feb 23 2025, jijini Dar es Salaam kujadili agenda sita.
Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam, Sabra Masanza ambaye ni Katibu wa Katibu Mkuu wa Chama hicho, amefafanua kwamba kamati hiyo moja ya agenda itakayojadili ni kutathmini hali ya kisiasa nchini baada ya uchaguzi.
Agenda nyingine ni kutathmini kwa kina uhai wa chama nchini, baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji, na Vitongoji.
Pia itajadili maandalizi ya Halmashauri Kuu kwa ajili ya kuitisha Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa na agenda nyingine ni Kuandaa na kupanga ratiba ya kuchagua wagombea wa nafasi mbalimbali za uwakilishi ndani ya chama, ikiwemo nafasi za udiwani, ubunge, na urais wa Zanzibar, na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sabra, ameongeza kuwa pia watajadili amani ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu na mengineyo yatokanayo na mkutano huo.
No comments:
Post a Comment