NA MWANDISHI WETU
MASTAA wa
filamu, Jimmy Mafufu na Shamsa Ford wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
sasa wakiwa chini ya Taasisi ya Mabalozi wa Mama wanaanza ziara nchi nzima kutangaza
mafanikio ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakiwa na kaulimbiu ‘Asante Mama’.
Nyota hao
wa filamu nchini wameamua kujiunga CCM wakitokea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
wanakiri sababu kubwa ya kuchukua uamuzi huo ni kutokana na utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa na Dkt Samia ambayo inafanya taifa
kukua kiuchumi.
Mafufu akizungumza leo jijini Dar es Salaam amesema "tumeamua kujiunga CCM baada ya kubaini kupitia Serikali ya Awamu ya Sita imefanya makubwa kwa Watanzania tukiwemo wasanii ambao tumepewa mikopo ambayo imetusaidia kuinua kazi zetu.
“Licha ya
kwamba mimi na Shamsha tulikuwa upinzani, mikopo hiyo inayotolewa na Rais wetu
kwa wasanii haikutubagua, pia Serikali yetu imefanya mambo makubwa ikiwemo
utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo kama Barabara, Bwawa la Mwalimu Nyerere,
Reli ya SGR, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato, hayo ni sehemu yaliyotukusukuma
kujiunga CCM,” amesema.
Amesisitiza
kwamba tangu Rais Dkt Samia, aingie madarakani ajashindwa, ametekeleza miradi
yote iliyoachwa na marehemu Rais Dkt John Magufuli, hali ambayo imefanya
kutoona umuhimu wa kubaki upinzani.
Wasanii hao wameungana na wasanii wengine akiwemo Salum Mchoma (Chiki), Single Mtambalike ‘Richt Ritch’, Rashidi Mwishehe ‘Kingwendu’ Abdallah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’.
Wengine ni wa
muziki wa kizazi kipya akiwemo Boniventure Kabongo ‘Stamina, Juma Kassim ‘Nature
‘Sir Nature’, Amani Temba ‘Capt Temba, Richard Shauri ‘Ritch One’ na wengine na
lengo lao ni kutangaza miradi yote ambayo imetekelezwa chini ya Rais Samia.
Shamsa naye
amesema kwamba anajivunia kujiunga na CCM na kutoa wito kwa wasanii wengine
ambao wako katika vyama vya upinzani kujiunga na ccm ili kuunganisha nguvu ya
pamoja kutangaza miradi ya maendeleo ambayo imefanikisha kustawisha uchumi wa
Tanzania.
Pia Ritch Ritch ambaye ni diwani wa CCM , amesema kuwa yeye ndiye kiongozi wa madiwani wote hivyo anaamini watatangaza, miradi yote ambayo imefanya vizuri kwa maslahi ya watanzania ili kila mmoja ajue namna Serikali ilivyofanikiwa kupitia miradi ya Elimu, Usafiri wa Anga na mingineyo inayofanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa katika mataifa mengine.
No comments:
Post a Comment