NA MUSSA AUGUSTINE
MWENYEKITI Mstaafu wa Kitengo cha Wanawake katika Taasisi ya Wahandisi,(IET), Mhandisi Upendo Haule, ametoa wito kwa Wanafunzi wa kike ngazi ya msingi hadi vyuo vikuu kupenda kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kuwa Wahandisi
Mha. Upendo qmetoa rai hiyo leo Februari 28,2025 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Wahandisi na Uhandisi Duniani yatakayo fanyika Machi 4,2025 ambapo Kitaifa yatafanyika mkoani Arusha.
"Kitaifa kutakua na Mkutano Mkuu ambao utafanyika mkoani Arusha ambapo umeandaliwa chini ya Wizara ya Ujenzi"amesema
Nakuongeza kuwa "Lakini sambamba na hilo upande wa Taasisi ya Wahandisi,tutakua na Kongamano ambalo tutalifanya hapa Dar es salaam katika Chuo cha Teknolojia Dar es salaam (DIT) likihusisha vyuo mbalimbali na wahandisi wanaoweza kushiriki.
Aidha Mhandisi Upendo ambaye pia ni Mhandisi mbobezi wa mradi wa Mkongo wa Taifa kutoka Kampuni ya Mawasiliano Nchini Tanzania( TTCL) amesema kuwa lengo kubwa la kongamano hilo ni kuhabarisha umma pamoja na wanafunzi wa vyuo kuonesha umuhimu wa uhandisi na kusherehekea sherehe ya Wahandisi na uhandisi Duniani.
Amesema kuwa Kongamano hilo litakua na mawasilisho mbalimbali yatakayokua yanazungumzia Wahandisi na teknolojia mbalimbali zinazoendelea za uhandisi.
"Sambamba na hilo tutakua na maadhimisho mengine maeneo mbalimbali ambayo yataendana na kutembelea shule (school Visit), kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi wa uhandisi" amesema
Nakusisitiza kuwa "Tumeamua kufanya Kongamano hili pale DIT na sio sehemu nyingine kwa lengo la kuhamasha uhandisi na kuwaonesha sisi wahandisi tuliopo lakini pia kuwahamasisha Wahandisi waliopo vyuoni kusoma kwa BIDII ili kufikia malengo.
"Tumeamua kwenda kwenye vyuo ili wao watuoneshe wanafanya nini,na sisi pia tuwaoneshe tunafanya nin,lakini mwisho wa siku tuweze kuhakikisha tunaongeza wahandisi."
Ameaema kwamba katika maadhimisho hayo ya Siku ya Wahandisi na Uhandisi Duniani, watatembelea shule za msingi na sekondari ili kuweza kuwaibua nakuwafanya wakae sawa kupata uelewa mzuri ili wasiache masomo ya sayansi.
"Kauli mbiyu ya Mwaka huu kwa mujibu wa kimataifa ambayo ipo chini ya UNESCO, "shaping our future through engineering"maana yake nikuhakikisha kwamba tunakua na dunia endelevu yenye kustahimimili kupitia uhandisi" amesema
Nakuongeza kuwa "yaani Dunia yetu ya Sasa itakuaje hapo baadae kupitia uhandisi?..,Je uhandisi tunaoufanya ni stahimilivu?..,Je upande wa Mazingira ususani uhandisi tunaoufanya unalinda Mazingira?..,Mitambo tunayoizalisha inalinda Mazingira?..maana yake ni kwamba huu uhandisi wetu usiharibu Mazingira".
No comments:
Post a Comment