NA BAKARI LULELA
WAKALA wa vipimo Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam wamekamata wafanyabiashara wawili ambao wamekutwa na tuhuma ya kutumia mizani isiyosahihi kutokana na kupunja uhalali wa vipimo.
Hayo yamebainishwa leo Machi Moshi, 2025 jijini Dar es Salaam na Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Kinondoni, Lilian Mwombeki, na kubainisha kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kufanya ukaguzi wa kawaida wa kushtukiza kulingana na Sheria ya vipimo sura namba 340 pamoja na mapitio yake ya mwaka 2002 na kubaini changamoto za baadhi ya wafanyabiashara ambao si waadilifu kutumia mizani isiyo kuwa na sifa kutoa huduma kwa wateja.
"Tukiwa katika ukaguzi wa mabucha ya nyama maeneo ya Mbezi Louis kwa Musuguli, Dar es Salaam, tulinunua nyama kilo 1 katika bucha la kwanza ambapo tulipata gramu 700 ambapo ilikuwa na mapungufu ya gramu 300,", amesema Lilian
Aidha meneja huyo ameeleza kuwa waliponunua bidhaa hiyo kwenye bucha la pili kwa kiasi cha kilo 2 ikaleta gramu 1600 badala ya gramu 2000 ambapo ilionekana imepunjjwa kwa gramu 400 hii imeonekana kwamba mizani mingi huwa haizingatii uhalali wa vipimo kwa wateja ambao ndio watumiaji wa bidhaa hiyo.
Hata hivyo kulingana na utaratibu wa Sheria za Wakala wa vipimo hufanya ukaguzi mara moja kwa mwaka na kaguzi wa kustukiza mara kwa mara hivyo wafanyabiashara hao wameshikiliwa kutokana ubadhilifu wa kutumia vipimo visivyo halali kwenye bidhaa halisia.
Alidai kuwa mara nyingi watu hao wanapowakamata hufuata utaratibu wa uhakiki wa bidhaa yenyewe na kipimo husika kwa kubaini ujazo na uzito vinaendana ama haviendani.
Hivyo watu hao ambao hukiuka Sheria za vipimo kwa makusudi kabisa hivyo huwashitaki kwa kuwalipisha faini au hupelekwa mahakamani kutokana na tatizo husika.
No comments:
Post a Comment