![]() |
NA SAIDI LUFUME, NJOMBE
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wadau wa uzalishaji mazao ya misitu kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao hayo hapa nchini badala ya kusafirisha malighafi hizo nje ya nchi.
Amebainisha hayo Machi 21, 2025 mkoani Njombe katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Upandaji Miti Kitaifa ambapo Rais Samia amepewa Tuzo ya Mageuzi katika Misitu, Uhifadhi
Amesema wakati umefika kwa Tanzania kunufaika na raslimali za sekta ya misitu kwa kuongeza thamani ya mazao ya misitu hapa hapa nchini hivyo kuinua uchumi wa nchi.
Aidha, amefafanua kuwa misitu ina mchango mkubwa katika uhifadhi wa wanyamapori, ufugaji nyuki, utalii, kilimo, upatikanaji wa maji kwa matumizi nyumbani, viwandani na mashambani pamoja na kuleta mvua.
Majaliwa amesema Tanzania ina eneo la misitu lenye ukubwa wa hekta milioni 48.1 sawa na asilimia 55 ya eneo la nchi kavu. Katika eneo hili hekta milioni 44.7 ikiwa ni asilimia 93 ni misitu ya uoto wa miombo na hekta milioni 3.4 sawa na asilimia 7 ni Misitu ya Uwanda wa Chini, Milimani, Mikoko na Mashamba ya Miti.
Pia Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuanzisha na kuendeleza programu mbalimbali za upandaji miti ambazo zitatekelezwa katika kipindi chote cha mwaka na sio kwa matukio tu, ili kuendelea kutunza mazingira.
Aidha amezitaka Mamlaka zote zenye jukumu la kulinda na kuhifadhi misitu zinakuwa na watalaam wa fani ya misitu ili kuboresha utoaji wa huduma za ugani hasa kwa wananchi walio vijiji.
Vile vile Wizara kuwa na mipango thabiti ya kukabiliana na moto wa misitu ikiwa ni pamoja na kuanza kutumia teknolojia katika kutambua na kupambana na moto.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema Wizara kupitia Wakala wa Misitu Tanzania ( TFS) tangu mwaka 2020 hadi sasa, mabapo amesema jumla ya miti 146,007,298 ya miti jamii mbalimbali ikiwemo mikoko 1,184,091 imezalishwa na kuoteshwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini huku akisisiiza kuwa tangu mwaka 2020 hadi sasa, TFS imefanikiwa kupanda jumla ya miti 146,007,298 ya miti jamii mbalimbali ikiwemo mikoko.
“Miche 50,063,665 ilipandwa katika maeneo yenye hekta 11,985.7 za mashamba ya miti ya Serikali na miche mingine (61,190,886) ilitolewa kwa jamii, taasisi, mashirika, watu kazi hii kubwaime imefanywa chini ya uongozi imara wa Samia Suluhu Hassani akisaidiwa na wewe Waziri wetu Mkuu ambapo miongozo na maelekezo yenu yametuwezesha kusimamia na kuendeleza rasilimali za misitu nchini.” amesema Waziri Chana
Machi 21, kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine duniani katika kuadhimisha siku ya misitu na upandaji miti ikiwa ni maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2012 kuadhimisha siku hiyo, lengo likiwa ni kuhamasisha jamii juu ya kutunza na kuhifadhi misitu na upandaji miti ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yameadhimishwa Mkoani Njombe kwa namna tofauti ikiwemo upandaji miti katika halmashauri nne maonesho ya Wanyamapori hai na waliokaushwa na mdahalo wa wataalamu wa sekta ya Misitu na Nyuki.
Maadhimisho hayo ya kitaifa ambayo yamehudhuriwa na maelefu ya wananchi na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, Naibu Waziri wa Utalii, Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi yameshuhudia pia maonesho ya teknolojia na bidhaa mbalimbali za misitu na utalii.





No comments:
Post a Comment