NA MWANDISHI WETU
SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, imetoa tamko la kupiga marufuku mazao ya kilimo kutoka Nchi za Afrika Kusini na Malawi baada ya Nchi hizo mbili kuzuia mazao kutoka Tanzania.
“Wakati mazungumzo yanaendelea sisi hatuwezi kuendelea kuishi kuzuiliwa haki yetu hiyo hivyo natangaza rasmi kuanzia usiku huu mambo yafuatayo kwa Nchi hizi mbili South Africa imekua ikiingiza Tanzania ‘fresh apples’ kwa hivyo kuanzia leo ni marufuku kuingiza fresh apples Tanzania hatutaruhusu zao lolote kutoka South Africa linalohusina na kilimo kuingia Nchini kwetu”
“Kuhusu Nchi ya Malawi mpaka sasa hawajafuta notisi waliyoitoa kwa hivyo ninatangaza rasmi ni marufuku mazao yoyote ya kilimo kutoka Malawi kuingia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia leo” amesema Bashe.
Kwa mujibu wa MilladAyo Update, Kaul hiyo ya Serikali ilitolewa na Waziri Bashe, Aprili 23, mwaka huu.
Chanzo, MilladAyo Update
No comments:
Post a Comment