KIONGOZI MBIO ZA MWENGE APONGEZA UJENZI WA BARABARA YA PICHA YA NDEGE-BOKOMNEMELA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, April 3, 2025

KIONGOZI MBIO ZA MWENGE APONGEZA UJENZI WA BARABARA YA PICHA YA NDEGE-BOKOMNEMELA




NA MWANDISHI WETU, PWANI

MWENGE wa Uhuru umeridhishwa na mradi wa ujenzi wa barabara ya Picha ya Ndege-Bomotimiza yenye urefu wa mita 550 kiwango cha lami wenye thamani ya shilingi milioni 760.


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ismail Ussi akikagua barabara hiyo ambapo fedha hizo nikutoka serikali kuu kutokana na tozo ya mafuta amesema serikali inapenda wananchi wapate miundombinu mizuri.


Ussi amesema kuwa kutokana na mradi huo kuwa na ubora wananchi wanapaswa kuulinda na kuutunza ili ulete manufaa ya muda mrefu na kuufanyia usafi.


Amesema kuwa serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kutengeneza miundombinu ambapo mradi huo umejengwa kwa viwango vinavyotakiwa kutokana na usimamizi mzuri.


"Rais Dk Samia Suluhu Hassan anapenda kuona miradi kama hii inakuwa na matokeo mazuri kwani ndiyo malengo ya serikali hivyo ulindeni mradi huu ambao una gharama kubwa,"amesema Ussi.


Kwa upande wake Mhandisi Samwel Ndoveni amesema kuwa mradi huo ulianza Oktoba mwaka 2023 na ulitegemewa kukamilika Aprili 2024 lakini muda uliongezwa na kukamilika Julai 2024 kutokana na mvua za elnino.


Ndoveni amesema kuwa mradi huo kwa sasa uko katika kipindi cha matazamio hadi Julai 2025 na kukabidhiwa rasmi na kuwa kiasi kilicholipwa hadi sasa ni shilingi milioni 696.9 sawa na asilimia 91.7.


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye ni Diwani wa Kata ya Sofu, Mussa Ndomba amesema kuwa barab8ara hiyo ambayo inaanzia barabara ya Morogoro ina urefu wa kilometa saba ni muhimu sana.


Ndomba amesema kuwa barabara hiyo inapita kwenye maeneo ya Shule, Magereza na Hospitali na inaunganisha Kata tatu za Sofu, Picha ya Ndege na Bokomnemela ambapo zamani ilikuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.




No comments:

Post a Comment