NA MWANDISHI WETU
CHAMA cha National League for Democracy (NLD) kinawataarifu wanachama wake, wapenzi wa demokrasia na wananchi wote kwa ujumla kuwa, baada ya mchakato wa ndani wa chama kukamilika kwa mafanikio, chama kimewapitisha rasmi wagombea wake wa nafasi za juu katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025.
"Kwa heshima kubwa, tunatangaza kwambao Doyo Hassan Doyo ameteuliwa rasmi kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha NLD.
Pia Mfaume Khamis ameteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama chetu," imesema.
Uamuzi huo umetokana na vikao halali vya chama, kufuata taratibu zote za kikatiba, na mapendekezo ya wajumbe wa mkutano mkuu kutoka sehemu mbalimbali kote nchini.
Taarifa ya chama hicho imesema kwamba ina imani kubwa kwamba viongozi hao ni mfano wa uongozi bora, wenye maono makubwa ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa Watanzania wote na NLD kimejidhatiti kuendeleza misingi ya demokrasia, uzalendo, haki, na maendeleo jumuishi kwa kila mtanzania.
No comments:
Post a Comment