KATIBU Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara, (kulia) akiwa na Mwenyekiti wake, Betha Mpata.
NA MWANDUSHI WETU
KATIBU Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara amepitishwa kuwania nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama hicho kwa kura 75 kwa upande wa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar, Ally Mwalimu Abdallah atasimama kuwania nafasi hiyo.
Uchaguzi wa kupitisha majina hayo umefanyika leo Aprili 28, 2025 kupitia Mkutano Mkuu jijini Dar es Salaam ukiudhuriwa na wajumbe 103 kutoka mikoa 18 ya Tanzania Bara na Zanzibar na kushuhudiwa na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza.
Wagombea wote kwa pamoja baada ya kuchaguliwa kuwania nafasi hiyo, walisisitiza kufanya kampeni za kistaarabu na kuendelea kudumisha amani na utulivu ili iliyojengwa tangu uhuru na wakatoa wito kwa viongozi wengine wa vyama vya siasa kudumisha amani na utulivu na kuacha uchochezi utakaosababisha vurigu nchini.
“Hii ndio nchi yetu, hatuna nchini nyingine hivyo tunapaswa watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyetu kuhamisisha amani katika kipindi hiki cha uchaguzi kwani tumeshuhudia nchi mbalimbali zikiharibika na kurejesha utulivu ni kazi kubwa,”wamesema.
Awali Mwenyekiti wa chama hicho Betha Mpata, wakati akitoa nasaha kwa wagombea aliwasisitiza watanzania kutosikiliza sauti za wanasiasa wanaochochea vurugu kwa maana hao nia yao ni ovu ya kutaka kuliingiza taifa kwenye machafuko huku wao wakiwa na sehemu ya kukimbilia, hivyo wapuuzwe.
“Nawaomba watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi msiwasikilize wanasiasa wachochezi kwani amani ikishaharibika wao watakuwa na sehemu ya kuimbilia nasi wengine tutaangamia hivyo tuwaapuze na tuendelee kujenga umoja na utulivu il tupite katika kipindi hiki cha uchaguzi tukiwa salama,” amesema.
Pia Nyahoza, kwa upande wake amekumbusha viongozi wa vyama vya siasa kwamba vina wajibu wa kulinda amani na utulivu iliyopo na kama kuna madai wanachotakiwa ni kutumia njia za kisheria ili kupata wanadai na si kuhamisisha vurugu ambacho kimsingi litafanya taifa kuingia katika machafuko.
“Najua kila chama msingi wake mkuu ni kushika dola na kutokana na hali hiyo kunakuwa na ushindani wa hali ya juu, hivyo licha ya ushindani kuwepo wanasiasa wanatakiwa kufuata utaratibu na sheria za nchi katika kufanikisha malengo yao na kuhakikisha wanatunza amani na utulivu uliopo,” amesema.







No comments:
Post a Comment