NA MWANDISHI WETU
ALIYEKUWA Kampeni Meneja wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, Tundu Lissu, Romanus Mapunda amejiunga rasmi na Chama Cha Wananchi (CUF).
Mapunda ametangazwa leo katika Ofisi za CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa CUF, Othuman Dunga.
Mapunda amesema amejiondoa CHADEMA kutokana na kuwepo Kwa mambo mengi yanayoendelea katika chama hicho ikiwemo udikteta na kutokubali kushauriwa kwa baadhi ya viongozi wakiwemo Lissu.
"Tulimwambia Lissu, hatuwezi kususia uchaguzi kwa maana njia hiyo itasaidia kupata reforms tunazozutaka, kwa maana tukiwa nje tutashindwa kupata madai yetu ikiwa tutasusia uchaguzi" amesema.
"Leo, nimejiunga CUF, nawaomba wanacuf, mjiandae kuwapokea wengine, muda si mrefu, pia ndoto yangu ya kuwania Urais ipo palepale, muda kufika nitagombea, mimi ni mtu wa kazi, majimbo yote ambayo yamelala tutayaamsha, tutatembea Kata Kwa Kata kupeperusha bendera ya CUF," amesema.
No comments:
Post a Comment