NA MWANDISHI WETU
JUMLA ya mawaziri 20 kutoka nchi mbalimbali duniani wameudhuria mkutano 18 unaofanyika kwa mara ya pili Tanzania unaohusu elimu mtandao (eLearning Africa).
Mkutano huo wa eLearning Africa ni heshima kwa nchi yetu wenye lengo la kubadirishana mawazo na uzoefu jinsi ya kutumia Digital System kwa ajili ya utoaji masuala ya Elimu ,
Akizungumza katika mkutano ndani leo Mei 7,2025 unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutayo ya Kimataifa wa Julius Nyerere (JNCC )Jijini Dar es Salaam , Profesa Adolf Mkenda amesema Tanzania wanajitaidi sana kutumia Mfumo wa elearning pamoja na kwamba hawajasambaza vya kutosha pia kuna njia za kutosha kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali yasio ya Kiserikali ili shule mbalimbali ziweze kufikiwa .
"Nchi yetu leo imepata heshima ya mkutano mkubwa wa 18 wa eLearning Afrika kufanyika na uliohudhuriwa na Mawaziri 20 kwa ajili ya kubadirisha mawazo pamoja na uzoefu" alisema Profesa Mkenda
Profesa Mkenda alisema watakikisha shule nyingi zinafikiwa na mfumo wa TEHAMA kwa ajili ya kujifunza kompyuta na walimu wote wapewe vishikwambi kwa ajili ya kusomea kwa sababu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alitoa agizo walimu wote wapatiwe Vishikwambi..
Aidha, alisema elimu mtandao ni nyenzo muhimu ya kufundishia pia sisi wenyewe tuwe na teknolojia ya akili mnemba ambapo alisema Serikali imeruhusu shule kuanzishwa Zanzibar na mfumo huo utachukua wanafunzi watakaojifunza.
Pia alisema kozi kama hizo zinatolewa katika chuo kikuu cha Dodoma na Nelson Mandela Arusha lakini pia bajeti ya mwaka huu wanafunzi wa kidato cha sita wanaofanya mitihani sasa hivi watakapata ufadhili wa masomo kama hayo.








No comments:
Post a Comment