RAIS DKT SAMIA KUZINDUA MRADI MPYA WA KUENDELEZA MISITU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 14, 2025

RAIS DKT SAMIA KUZINDUA MRADI MPYA WA KUENDELEZA MISITU


NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajia kuzindua mradi mpya  wa kuendeleza misitu unaoagharimu Shilingi mil 40 anatarajiwa kuuzindua hivi karibu jijini Dar es Salaam.

Dkt Hassan Abbas Katibu Mkuu wa Wizara ya Mali Asili na Utalii, amebainisha hayo leo jijini Dar es Salaam wakati Mke wa Rais WA Finland, alipotembelea Makumbusho ya Taifa, Posta jijini humo.


Pia ametanabaisha kwamba, fedha hizo zitakuwa kichocheo kizuri cha kuendeleza misitu nchini na kutokana na ushirikiano mazuri na Taifa la Finland wataendelea kubadilisha wataalam katika nyanja hiyo kuleta ufanisi unaokusudiwa.

"Nchi yetu imekua na mashirikiano makubwa na nchi ya Finland kwani sisi ni marafiki wa muda mrefu ambapo hata Rais Hayyat Mwl Julius Nyerere miongoni mwa ziara zake za mwaka 1973 alitembelea nchini Finland"


"Sisi wizara ya mali asili na utalii tunanufaika sana na wenzetu wa Finland hasa katika sekta ya misitu, tuna ushirikiano wa zaidi ya miaka 40, miradi ambayo tumekuwa tukiifanya inayohusu misitu na mazao yake, huu mradi ambao tutausaini kesho kutwa ni mwendelezo wa haya yote ambayo wamekuwa wakitusidia"


Katika ziara hiyo fupi ya Mke wa Rais wa Finland kutembelea Tanzania pia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hivi karibuni atazindua mradi wa Pound mill 20 sawa shilingi mill 40 za Kitanzania ambao ni  mradi mpya utakaosaidia kukuza na kuendeleza sekta ya misitu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema ujio wa Mke wa Rais, Finland ni mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuutangaza utalii lakini pia ni alama kwa Wizara ya mali asili na utalii katika kupanua wigo wa kutangaza vivutio vya utalii.


Ameongeza" Hii sasa ni hamasa kwa watanzania  na wageni waendelee kutembelea makumbusho ya taifa kwa ajili ya kujifunza historia ya taifa, utamaduni na urithi, kufahamu muingiliano wa nchi hii na mataifa mengine na mashirikiano mazuri baina ya nchi na mataifa mengine..."


Aidha, amesema makumbusho ya taifa wanashughulika na tafiti ukusanyaji, uendelezaji na kutoa elimu kwa Jamii, hivyo wangependa kushirikiana na nchi ya Finland katika katika kufanya utafifi katika eneo la tamaduni na mali kale kwani wao wamepiga hatua katika eneo hilo.


Hata hivyo, amesema ujio wa Rais wa Finland kesho pia kutembelea makumbusho ya taifa si tu kuacha alama mashirikiano mazuri yaliopo baina ya nchi hizo mbili bali kuwakumbusha watanzania kupenda na kuthamini vitu vya kwao.





No comments:

Post a Comment