NA MWANDISHI WETU
WAFANYABIASHARA wazawa, wadau katika sekta ya madini na Chama Cha Wachimbaji Wadogo wa Madini wametakiwa kujiunga na Taasisi ya Usambazaji Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA) kwa lengo la kuwa na sauti moja katika kufikia malengo.
Sebastian Ndege ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano TAMISA, ametoa wito huo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Kongamano litakalofanyika Mei, 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Amefafanua kuwa siku hiyo licha la kufanyika kongamano litakalojadili changamoto na namna ya kuzifikia fursa zilizoko kwenye sekta ya madini, pia Kamati ya Mawasiliano itazinduliwa rasmi.
"Mgeni rasmi katika kongamano hilo ambao pia litatumika kuzindua Kamati ya Mawasiliano likakalokuwa na jukumu la kuhabarisha umma na wadau wa sekta hiyo juu ya fursa zinazoweza kupatikana kupitia sekta ya madini kupitia Website na makongamano atakuwa Waziri wa Madini Antony Mavunde" amesema.
Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Peter Kumalilwa akifafanua jambo.
Naye Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Peter Kumalilwa amesema kwamba katika uongozi amejipanga kazi kubwa mbili, moja ni kuhakikisha kunakuwepo na viwanda vya wazawa vinavyohusiana na madini na kuhakikisha Shilingi trillion 3.1 zinazotolewa na kampuni kubwa za madini hapa nchini wazawa wachangie zaidi ya asilimia 20 au zaidi jambo ambalo watakuwa wakijivunia kama Watanzania.
Pia alitoa shukrani zake Kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuifungua sekta ya madini katika soko la kimataifa na kuweka mikakati ya kuhakikisha wazawa wanapiga hatua kuweza katika sekta hiyo hapa nchini.
Ameongeza kuwa TAMISA itakuwa na majukumu kadhaa ikiwemo kuhamasisha wazawa kufungua vya madini, kuhabarisha wadau hususani wazawa fursa zinazopatikana kupitia sekta hiyo sanjari na kuwaunganisha wadau wazawa kuwa sauti moja na kufikia mafanikio yanayohitajika.

.png)




No comments:
Post a Comment