WAZIRI MHAGAMA ATOA ZAWADI KWA MWANDISHI BORA WA MAKALA SEKTA YA AFYA 2025 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, May 6, 2025

WAZIRI MHAGAMA ATOA ZAWADI KWA MWANDISHI BORA WA MAKALA SEKTA YA AFYA 2025


NA MWANDISHI WETU - WAF

WAZIRI wa Afya,  Jenista Mhagama amekabidhi tuzo, cheti na zawadi ya Shilingi Milioni 5 tasilimu pamoja na pikipiki mpya kwa Mwandishi Bora wa Habari, Ismaily Kawambwa  ambaye ameshinda tuzo ya Uandishi Bora wa Makala ya Sekta ya Afya  Kwa Mwaka 2025.


Zawadi hiyo imetolewa leo Mei 5, 2025 jijini Dar es Salaam katika hafla ya Samia Kalamu Awards iliyoandaliwa na Chama cha waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa  kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)  


Katika Hafla  hiyo ambayo mgeni Rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imewashirikisha viongozi mbalimbali wa Serikali, wamiliki wa vyombo vya habari na waandishi wa habari.


Lengo la tuzo hizo ni kuhamasisha uandishi wa habari zinazohusu maendeleo pamoja na utekelezaji wa sera za Serikali na kuwafikia wananchi kupitia vyombo wanavyoviwakilisha.




No comments:

Post a Comment