NA MWANDISHI WETU
SALUM Ismail, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Vyuo Vikuu Mkoa wa DODOMA ametangaza kutia Mia kuwania Ubunge katika Jimbo la Kahama Mjini mkoani Shinyanga.
Amesema wazi hayo leo Juni 18, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kufafanua kwamba lengo la kuwania nafasi hiyo ni kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fursa ya uongozi kwa vijana.
Amefafanua kuwa anaamini kwamba kuwania kwake uongozi utakuwa ni sehemu ya kuwaketea maendeleo wananchi jimbo hilo wakiwemo wanaofanya migodini.
Hivyo amesema kuwa Juni 28 Mwaka huu atakuwa ni miongoni mwa wagombea watakao jitokeza kuchukua fomu.
Katika hatua nyingine Salum amekemea wanasiasa na wanaharakati wanaochochea uvunjifu wa Amani Nchini hivyo amesema kuwa watahakikisha wanapambana nao.
Aidha ametoa wito kwa Watanzania kumuunga mkono Rais Samia kutokana na mazuri aliyoyafanya.
Kwamba Wakati anapokea kijiti Cha uongozi baada ya kifo cha Rais Dkt. John Magufuli kulikuwa na miradi mingi ambayo ilikuwa ikiendelea.
Amesema kuwa kutokana na Mazingira hayo watu wengi walidhani Rais Samia asingeweza kuiendeleaa na kuikamilisha, hata hivyo ameitekeleza vizuri na kuikamilisha jambo ambalo linafanya Watanzania wamuunge mkono.
Amekemea watu wanaomkejeli na kumsema vibaya kwamba hawatawavumilia.
No comments:
Post a Comment