DC KASILDA AIPONGEZA HALMASHAURI KUTOA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA WAKATI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, June 27, 2025

DC KASILDA AIPONGEZA HALMASHAURI KUTOA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA WAKATI


NA MWANDISHI WETU 

MKUU wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa kutoa  mkopo wa asilimia 10 za mapato ya ndani kwa wakati ili kuwainua wananchi kiuchumi.


Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya wakati akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni 210 ambazo ni Mkopo wa robo ya nne  kwa wanawake ,Vijana na watu wenye ulemavu.


"Nimpongeze Sana Mkurugenzi kwa kuhakikisha kuwa Mkopo huu unatolewa kwa wakati"alisema Mheshimiwa Kasilda


Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Jimson Mhagama amewataka wanufaika wa mkopo kuhakikisha kuwa wanarejesha fedha hizo kwa wakati.


"Serikali imewaamini hivyo hamna budi kuimarisha imani yenu kwa Serikali kwa kurejesha kwa wakati"amesema Mhagama



Kwa upande wake Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Same, Anatoly Charles amesema jumla ya vikundi 36  vimenufaika na Mkopo huo ambapo vikundi 24 ni vya wanawake,Vijana ni vikundi 9 na watu watatu wenye ulemavu.


Amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Same imetoa Mkopo wa Shilingi Milioni 585.5 kwa vikundi 113.

No comments:

Post a Comment