MWANDISHI WETU
DK Ally Njama kutoka Halmashauri ya Ubungo amefanikiwa kurejesha fomu ya kutia nia kugombea Jimbo la Ubungo katika Uchaguzi Mkuu ujao Oktaba mwaka huu.
Kada huyo aliyewahi kuhudumu kwa mafanikio makubwa akiwa Hospitali ya Mwanachana, amebainisha kuwa Kwa kufanikisha hatua hiyo kikubwa ni kumshukuru wadau kwa kumuombea na MwenyeziMungu kwa kumfikisha katika hatua hiyo.
"Ni leo ikiwa siku ya mwisho ya kurudisha fomu, nashukuru Mungu kufanikiwa kurejesha fomu ya kutia nia kugombea ubunge katika Jimbo hili la Kibamba.
"Sasa hatua iliyobaki ni kuwaachia wajumbe wafanye kazi yao na jina langu likirudi nitashukuru na ndio utakuwa mwanzo wa safari kuelekea kwenye uchaguzi na ndio nitasema vipaumbele vyangu", amesema
.png)




No comments:
Post a Comment