MHANDISI Noah Mahimbo (SANYANGASI) amerejesha fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Mvomero Morogoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akiongea baada ya kurejesha fomu Mhandisi Mahimbo ameahidi kushirikiana na Rais Dk Samia Suluhu Hassan na viongozi na wananchi wote wa Mvomero katika kutekeleza ilani ya (CCM) ya 2025-2030 lakini pia katika Kuifanya Mvomero kuwa Mvomero ya Viwanda.
Sanyangasi amesema kuwa endapo akipata ridhaa ya kupeperusha bendera katika Uchaguzi Mkuu na kuwa Mbunge ajenda yake kuu ni kuifanya Mvomero kuwa wilaya ya wazalishaji kwa kuwekeza katika kilimo biashara ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment