MGOMBEA UBUNGE ANUSURIKA KIFO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, July 31, 2025

MGOMBEA UBUNGE ANUSURIKA KIFO

* NI BAADA YA GARI LA KUNG'OLEWA NATI


NA MWANDISHI WETU, MWANGA


KATIKA kile kinachodaiwa ni vita ya kutafuta ubunge katika Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro, leo watu wasiojulikana wamedaiwa kung'oa nati za mbele za gari ya mgombea ubunge, Shaibu Mruma.


Tukio hilo limetokea leo Julai 31.2025 akiwa katika Kata ya Mgagao ambapo wagombea wa ubunge kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani hapo wameanza kampeni ya kuomba kura kwa


wajumbe wa chama hicho, kabla ya Agosti 4 kupigiwa kura.


Mruma amesema anahisi gari yake imefunguliwa nati za mbele walipokuwa wanajitambulisha na kujinadi kwa wajumbe.


"Tukio hilo limetokea leo tulipokuwa tumetokea kata ya Mgagao kuelekea kata ya Kiria ambapo baada ya kuona mtikisiko (webling) kwenye gari katika steling na mlio ilibidi nisimamishe gari kukagua ndio tulipogundua kwamba nati zote za matairi ya mbele zimefunguliwa," amesema.


Hata hivyo Mruma amesema hakuna madhara yeyote kwa mgombea wala mtu mwingine kutokana na kadhia hiyo.


No comments:

Post a Comment