WADAU WA UVUVI, WACHAKATA SAMAKI WAHAMASISHWA KUJIUNGA TAOME - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, July 14, 2025

WADAU WA UVUVI, WACHAKATA SAMAKI WAHAMASISHWA KUJIUNGA TAOME

 


NA MWANDISHI WETU

WADAU wa biashara ya samaki wa bahari na maji baridi, wameombwa kujiunga katika wa wafanyashughuli hizo (TAOME) ili kupata fursa ya ambazo zipo serikalini na kwa wadau wengine wa maendeleo itakayowasaidia kufikia malengo mahususi.

 

Akizungumza  mwishoni mwa wiki iliyopita katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2025), Meneja Biashara  wa Reuna Group Of Company, Alex Kamshana , ambaye pia ni Mwanachana wa TAUME, amefafanua kwamba ikiwa wadau hao  wtajiunga katika umioja huo wataweza kufikia malengo kwa haraka.

 

“Wadau na wafanyabishara ya samaki tukijiunga kwa wingi katika umoja huu, itatufanya kuzisogelea fursa zilizopo serikali na wadau wengine wa maendeleo na wataweza kutusaidia mahitaji mbalimbali ili malengo yetu, kutokana na changamkoto zinazotukabili.

 


“Pia kila mdau atakuwa na mawazo yake katika kufikia mafanikio kupitia biashara hii, hivyo tukiunganisha mawazo tofauti, tunawekuwa na nguvu ya pamoja katika utatuzi wa changamoto zilizopo katika sekta hii na kupiga hatua kubwa kimaendeleo,” amesema.

 

Ameongeza kuwa soko la biashara hiyo, linaushindani mkubwa kutokana na uwepo wa wawekezaji wa nje ambao wamekuwa wakitumia vifaa vyenye uwezo mkubwa wa kuvulia samaki katika kina kirefu ikiwemo meli za kisasa.

 

Amebainisha kwamba ili ukifike ndoto katika jambo linalohitaji watu ni busara kuungana  na wenzako, hivyo ikiwa wadau hao kwa wingi wao watajiunga katika umoja huo, Serikali na wadau wa maendeleo itawaangalia kwa karibu.

Akizungumzia kuhusu taasisi yao ya REUNA ambayo ipo Mkuranga mkoani Pwani, wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwanga mkono katika shughuli zao kwa kuwatia boti ya uvuvi .


"Tunamshukuru Rais wetu kutuunga mkono katika shughuli zetu,.Kwa kipindi hiki ushindani umekuwa mkubwa kutokana na kuja kwa wawekezaji kutoka nje ambao wamekuws zana mahiri , ombi letu kwa Serikali itupatie meli ya kisiasa itakayotusaidia kwenda kwenye maji ya kina kirefu,' amesema.



Akizungumzia samaki aina ya Kambakochi ambao wanapatikana kwenye mapango, ameiomba Serikali kufanya tafiti ili ipatikane mbegu itakayosaidia wafugaji kupata na kufuga kama ilivyofanya  Jongoo Bahari.


"Kwa sasa kilo moja ya Kambakochi ni anafiiia 150,000 kutokana na upatikanaaji wake kuwa haba, hivyo ikipatikana mbegu yake na watu kufuga itarahisisha upatikanaji wake," amesema.


No comments:

Post a Comment