WADAU
wa biashara ya samaki wa bahari na maji baridi, wameombwa kujiunga katika wa
wafanyashughuli hizo (TAOME) ili kupata fursa ya ambazo zipo serikalini na kwa wadau
wengine wa maendeleo itakayowasaidia kufikia malengo mahususi.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita katika Maonesho
ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2025), Meneja
Biashara wa Reuna Group Of Company, Alex
Kamshana , ambaye pia ni Mwanachana wa TAUME, amefafanua kwamba ikiwa wadau
hao wtajiunga katika umioja huo wataweza
kufikia malengo kwa haraka.
“Wadau
na wafanyabishara ya samaki tukijiunga kwa wingi katika umoja huu, itatufanya
kuzisogelea fursa zilizopo serikali na wadau wengine wa maendeleo na wataweza
kutusaidia mahitaji mbalimbali ili malengo yetu, kutokana na changamkoto
zinazotukabili.
“Pia
kila mdau atakuwa na mawazo yake katika kufikia mafanikio kupitia biashara hii,
hivyo tukiunganisha mawazo tofauti, tunawekuwa na nguvu ya pamoja katika
utatuzi wa changamoto zilizopo katika sekta hii na kupiga hatua kubwa
kimaendeleo,” amesema.
Ameongeza
kuwa soko la biashara hiyo, linaushindani mkubwa kutokana na uwepo wa wawekezaji
wa nje ambao wamekuwa wakitumia vifaa vyenye uwezo mkubwa wa kuvulia samaki
katika kina kirefu ikiwemo meli za kisasa.
Amebainisha
kwamba ili ukifike ndoto katika jambo linalohitaji watu ni busara kuungana na wenzako, hivyo ikiwa wadau hao kwa wingi
wao watajiunga katika umoja huo, Serikali na wadau wa maendeleo itawaangalia
kwa karibu.
"Tunamshukuru Rais wetu kutuunga mkono katika shughuli zetu,.Kwa kipindi hiki ushindani umekuwa mkubwa kutokana na kuja kwa wawekezaji kutoka nje ambao wamekuws zana mahiri , ombi letu kwa Serikali itupatie meli ya kisiasa itakayotusaidia kwenda kwenye maji ya kina kirefu,' amesema.
Akizungumzia samaki aina ya Kambakochi ambao wanapatikana kwenye mapango, ameiomba Serikali kufanya tafiti ili ipatikane mbegu itakayosaidia wafugaji kupata na kufuga kama ilivyofanya Jongoo Bahari.
"Kwa sasa kilo moja ya Kambakochi ni anafiiia 150,000 kutokana na upatikanaaji wake kuwa haba, hivyo ikipatikanabegu yake na watu kufuga itarahisisha upatikanaji wake," amesema.
No comments:
Post a Comment